KILIMO BORA CHA MATANGO



Utangulizi
Matango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na hustawi vyema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C

Udongo 
Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji

Maandalizi ya shamba 
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45
Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta

Upandaji 
Zipo aina mbili za upandaji, 
  1. kupanda mbegu moja kwa moja na
  2. kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10.
Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi. Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda. Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei itatumika Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda

Palizi 
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu. Njia nyingine ni matumizi ya plastiki maalum kuzuia magugu yaani ‘plastic mulch’

Mbolea 
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda na kisha tumia NPK yenye uwiano mmoja kama, 18:18:18, 17:17:17 ama 16:16:16 baada ya wiki tatu toka Usegekaji. Tumia nguzo za unene wa inchi 2 na kamba ili kuinua mimea na matunda yasiguse ardhi na kuoza

Uchavushaji
Hii ni muhimu sana kuzingatiwa kwani tango huchavushwa kwa wadudu na si upepo. Bila wadudu kama nyuki uzalishaji huathrika sana. Ni muhimu kupanda mazao kama alizeti na maua mbali mbali yanayopendwa na wadudu wachavushaji ili kuhakikisha uwepo wa wadudu hao shambani. Aidha inapo-lazimu ni vema kuweka mizinga kadhaa ya nyuki katika shamba la tango

Matumizi ya viuatilifu Katika udhibiti wa wadudu na magonjwa matumizi ya viuatilifu yafanyike kwa maelekezo ya wataalam kubaini tatizo na kiuatilifu hitajika na namna ya matumizi yake

Mavuno 
Mavuno huanza baada ya siku 40 hadi 45 kutegemea na aina pamoja na hali ya hewa.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA