ALIYEMTUKANA RAISI MAGUFULI AKABIDHIWA MIL 4.5



Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akalipe faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu.

Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
 
Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini,  Diwani wa Levolosi,  Ephata Nanyaro amesema jana kuwa  wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha.

"Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, " amesema Nanyaro.

Naye,  Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za mitandaoni

Kwa hisani ya Mpekuzi blog

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA