ALEX MSAMA AMWANGUKIA MWAKYEMBE BAADA YA GAZETI LAKE LA DIRA KUCHAPISHA HABARI ZENYE UTATA
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki. Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagw a hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari. Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo. Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe. Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo. “Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachuk...