BUNGE LAJADILI KIPIGO CHA LIPUMBA MJADALA WOTE HUU HAPA



Leo Bunge Limejadili  hoja ya dharura ya Mh.Mbatia juu ya kupigwa kwa Mh.Lipumba wakati wa mkutano wake na wananchi wakati wa kumbukumbu ya mauaji ya wenzao waliokuwa wamefariki Pemba 2001.
 
Hoja hiyo imejadiliwa kwa mujibu wa kifungu cha 47  ambapo  msemaji  wa  kwanza  alikuwa  ni  Waziri  wa  Mambo  ya  ndani  ya  nchi ambaye  alisimama  kutoa  msimamo  wa  serikali.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Chikawe:Kufatia hoja ya Mh James Mbatia Mbunge ninamaelezo yafatayo, Tar 26 Jan Jeshi la polisi lilipokea barua kutoka Chama cha CUF. Barua hiyo ilikuwa ikitoa taarifa za kufanyika kwa maandamano kwenye viwanja vya Zackiem MBagara.
 
Maandamano yalipangwa kuanzia Temeke kuelekea Zackiem, Jeshi la polisi liliwaita viongozi wa CUF kwa mazungumzo. Walifanya mazungumzo na jeshi la polisi lilitoa tahadhari kadhaa kutokana na sababu za kiusalama. Viongozi wa CUF waliridhika na ushauri wa kamanda SIRO.
Katika hali ya kushangaza Profesa Ibrahimu Lipumba alikaidi Zuio la Jeshi la polisi na Kuamrisha wananchi kuandamana kuelekea Zackiem.
 
Jeshi la polisi linataka kila mtu kutii sheria bila shuruti, Na mtu yoyote akishindwa kufanya hivyo jeshi la polisi litamshughulikia mtu yoyote bila kujali umri, jinsia, wala madaraka yake.
 
Mwanasheria mkuu wa serikali:Jambo hili linaletwa bungeni ili bunge lijadili lifanye maamuzi, na limepelekwa mahakamani ili mahakama ilifanyie maamuzi.
 
Mamlaka yenye wajibu wa mwisho wa kutoa haki kwenye jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Mahakama.
 
Mheshimiwa spika naomba kushauri, kwenye mazingira kama haya 

bunge lako tukufu lisijadili jambo hili.

Spika Makinda: Hoja hii tunaijadili kwa dakika 3, namuita mchangiaji wa kwanza:

Hoja  za  Wabunge

Tundu Lissu: Kanuni zinasema tutumie dakika 15, haiwezekani waziri atumie dakika 30, na AG atumie 15 halafu sisi 3. Natumia 15
 
Spika Makinda: Haya basi tumieni dakika 10 na siyo 15, lakini tuzingatie tahadhari iliyotolewa na Mwanasheria Mkuu
 
Tundu Lissu: Huyu waziri wa mapolisi amesema uongo na hastahili kuwa katika nafasi kuanzia sasa
 
Tundu Lissu: Sasa tumejua kuwa ile kauli ya WAPIGWE TU ni kauli ya serikali na kauli ya CCM, jeshi la polisi ni la ma 'FACIST'
 
Tundu Lissu: Bunge lichukue hatua dhidi ya Polisi, waziri Mkuu, Waziri Chikawe, IGP naibu IGP. Tumechoka lazima wawajibike
 
Tundu Lissu: Tunahitaji tuunde tume teule kuchunguza matukio ya mapolisi kupigwa watu, tumechoka kupigwa
 
Tundu Lissu: Tukiendelea hivi na tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba, kumbukeni nyie ni wanachama wa mahakama ya Kimataifa ICC
 
Habibu Mnyaa: Pingamizi la jeshi la polisi lilikuja siku ya Maandamano tar 27 asubuh, na sio tar 22 kama inavyosemwa. Kwahiyo ni swala la kusikitisha na la aibu Waziri kuja kutoa kauli za uongo hapa bungeni ni jambo la kusikitisha sana. Profesa Lipumba alitii kauli ya mahaka na Taifa zima limeshuhudia kwenye vyombo vya habari.
 
Mbali na kutumia nguvu zisizostahili, Jeshi la polisi lilitumia Zana zisizoruhisiwa kwenye kazi yao, Jeshi la polisi lilitumia hadi wheel Spana.
 
Mkosamali: Kinachoendelea kwenye nchi yetu ni uvunjaji wa katiba, Ripoti ya common wealth (jumia ya madola) ilisema, Jeshi la polisi la Tanzania bado lina mifumo ya kikoloni ambayo lengo lake lilikuwa kuhakikisha Wakoloni wanabaki madarakani na waafrika hawaingii madarakani.
 
Leo mnachokifanya nyinyi CCM ni kufanya yeleyale waliyokuwa wanafanya wakoloni.

Nassari: "Doller yoyote inayotumia nguvu na mabavu kutawala, inafundisha kuwa Nguvu hiyohiyo itumike kuiondoa hiyo doller" Nelson Mandella.

Rashid Abdallah: Mauaji yanafanyika katika nchi hii, watu wanakufa, halafu jeshi la polisi lipo tu linaangalia
 
Rashid Abdallah: Waziri Mkuu bado anashabikia watu kuendelea kupigwa, Waziri hafai kuongoza wizara hii
 
Rashid Abdallah: Prof Lipumba ni sawa na Kikwete, wote ni wenyeviti wa vyama halali, haiwezekani afanyiwe vitendo kama vile
 
Mbowe: Nasikitika sana kwa taarifa aliyoitoa Chikawe, tupo kama serikali ilivyo kudharau na kuchukua taarifa ya upande mmoja
 
Mbowe: tarehe 27, nilipokuwa na Prof Lipumba, askari polisi waliniambia kuwa taarifa hii ya kupiga walipewa kutoka juu. Sitawataja
 
Mbowe: Mimi mwenyewe ni muhanga, nilishambuliwa na bomu, nikashambuliwa kwa Machine Gun na nikashambuliwa kwa bastola siku moja
 
Mbowe: Mnafurahi kwa kuwa hampigwi nyinyi, Rose Kamili alipigwa Iringa na watu wa CCM na Polisi mkafurahi, na sasa amekuwa kilema
 
Mbowe: Rose Kamili ameigharimu serikali zaidi ya milion 102 kwa matibabu nchini India, hamuoni hasara kwa taifa masikini kama hili.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA