DAMU,AGANO NA SADAKA
Agano ninini?
Agano ni mapatano au
makubaliano kati ya mtu na mtu, mtu na Mungu au mtu na mizimu.
Agano la Mtu na
mizimu
Agano hili hufanyika kwa njia ya damu na sadaka,
Mtu anapoenda kwa mganga wa kienyeji na kuchanjwa chale tayari ameshafanya agano
kwenye madhabahu ya mganga wa kienyeji ambaye ni wakala wa shetani. Hivyo
anapotoa ile damu tayari umeshajiunganisha na madhabahu ile wewe ni mtumwa wa
kuzimu hivyo huwezi kufanya jambo lolote bila idhini/ruhusa ya hao ‘’waliokununua‘’
kwa damu yako mwenyewe .
(KUTOKA 34:12)
Ujihadhari nafsi yako
usije ukafanya maagano na wenyeji wa nchi ile unayoiendea usije ukawa mtego
katikati yako.13Bali utabomoa madhabahu zao na kuvunja vunja kazi
zao na kuyakata maashera yao.15Usije
ukafanya agano na wenyeji wan chi watu wakaenda kufanya uzunzi na miungu yao na
kuitolea sadaka miungu yao mtu mmoja
atakuita ukila sadaka yake.
(WALAWI 17:11)
Kwakuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu,name nimewapa ninyi hiyo damu juu
ya madhabahu ili kufanya upatanisho juu ya nafsi zenu kwani ni hiyo damu
ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi .
Kwahiyo Kuokoka ni jambo moja, na kuvunja agano ni jambo lingine usije
ukajifariji kuwa ukioka umekuwa kiumbe kipya ya kale yamepita tazama yamekuwa
mapya .Hivyo hata kama umeoka huwezi kufanikiwa usipovunja agano na madhabahu
uliyomwaga damu yako
AGANO LA SADAKA KATIKA
MADHABAHU ZA KUZIMU LINAVYOWEZA KUKUZUIA
KUFANIKIWA
Watu wengi wanafanya
kazi kwa bidii na kupata pesa nyingi lakini mwishoni pesa zao kuisha bila wao
kujua hii inatokana na zile hela ulizokuwa unatoa kule kwa mganga wa kienyeji
kama nilivyosema awali kuwa ukisha fanya agano nao lazima watakufanya mtu wao
chochote utakachofanya ni kwa ajili yao hata pesa ukitafuta ni zao maana wewe
ni mtumwa wao
JINSI YA
KUJIKOMBOA NA KUJITOA KWENYE MADHABAHU HIZO
Kama ambavyo ulifanya agano kwenye madhabahu hizo kwa njia
ya damu na sadaka na wewe hiyo hiyo unatakiwa ujitoe huko kwa njia ya damu na
sadaka vile vile.
(WALAWI 16:6)
Na Haruni atatoa Yule Ng’ombe wa Sadaka kwa ajili ya dhambi zake, aliye
kwa ajili ya nafsi yake na kufanya
upatanisho kwa ajili ya nafsi yake yeye mwenyewe na Nyumba yake.
By Evangelist Prisca E Mwang'ombola
SOMO LINALOFUATA
JINSI MTU ANAVYOWEZA KUPATA LAANA NA MIKOSI KWA NJIA YA
KUJAMIIANA/KUZINI.
Comments
Post a Comment