JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

NA MWALIMU PRISCA MWANG'OMBOLA 



Nguvu za Mungu  hukaa kwa mtu anaye fanya maombi, huwezi kukaa  na nguvu za  Mungu kama wewe sio muombaji  maana ndio silaha kubwa ya  kuweza  kuzishinda hila za mwovu, kwa maana vita yetu haipo katika nyama na damu ipo katika roho na falme za wakuu wa giza. 

Unapokuwa na nguvu za Mungu unakuwa na unakuwa na faida zifuatazo

      1. Unakuwa na uwezo wa kushinda nguvu za giza
Nguvu za Mungu zinatupa kushinda nguvu zote za giza,  hivyo ni vyema kuhakikisha unatembea na nguvu za Mungu na kujilinda na Mambo yote yanayosababisha nguvu za Mungu kupungua au kuisha kabisa.

(EFESO 6:10-13 10 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. 
11 Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. 
12 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. 
13 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.)

      2.Unakuwa na mamlaka
Unapokuwa na nguvu za Mungu tayari nafsi yako inakuwa imeunganishwa na Mungu hivyo unamamlaka ya kuamuru chochote na kikafanyika sio kila kitu lazima kuombewa, unapoamua kumkiri Yrsu na kuwa Bwana katika maisha yako, uwezo na  mamlaka inakuwa mikononi  mwako
(MATHAYO 8:9-10  9  Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
10  Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.)

      3.Unakuwa na ulinzi.
Huwezi kuwa naulinzi kama hun nguvu za Mungu, nguvu za Mungu zinatulinda na mashambulizi ya kiroho yale ambayo hatuwezi kuyaona kwa Macho

 (ZABURI 125:2 2  Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.)
(ZABURI 27:1-6 1  Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
2  Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
3  Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.
4  Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake.
5  Mradi atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya, Atanisitiri katika sitara ya hema yake, Na kuniinua juu ya mwamba.
6  Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi Bwana.)

 4. Unakuwa na hofu ya Mungu
Nguvu za Mungu hutufanya tuwe na hofu ya kutenda dhambi na kumfanya mtu kuugua nafsi yake pale anapoenda kinyume ,
Kwamfano mtu anaposema uongo  kama ndani yako huna hofu ya Mungu utaona ni jambo la kawaida na pia mtu anaweza kujisifu kwa sababu Fulani ameamini uongo wakelakini ukiwa na hofu ya Mungu kamwe hutaweza kupata amani.

(KOLOSAI  3:9 -10 Msiambiane uongo, kwani ninyi mmekwisha vua ule utu wa kale pamoja na matendo yake yote, 10 mkavaa utu mpya. Huu unaendelea kurekebishwa na Mungu, Muumba wake, kadiri ya mfano wake, ili mpate kumjua Mungu kwa ukamilifu.)

      5. Unakuwa na imani
Yote kwa yote Imani ndio kila kitu, hakuna mtu anayeomba kitu pasipo kutarajia kupata hivyo hivyo katika maombi pia,  imani ndio ufunguo wa kila kitu yote,  matarajio ya mama mjamzito ni kupata mototo vivyo hivyo matarajio ya muombaji ni kupokea

(EFESO 6:16 Zaidi ya haya yote, jivikeni imani kama ngao ambayo itawawe zesha kuzuia mishale yenye miale ya moto kutoka kwa yule mwovu. )

     6. Nguvu za Mungu zinaimarisha uhusiano wetu na Mungu
Mawasiliano yetu na Mungu ni yanaimarishwa na uhusiano wetu mzuri nay eye, huwezi kuwa na mawasiliano na Mungu kana huna uhusiano nay eye, hata mzazi Nyumbani huwezi kuwa na mahusiano mazuri hata na mwanao wa kumzaa kama haenendi vile unavyotaka hivyo basi hata Mungu wetu pia huwezi kuwasiliana naye kama huna mahusiano  mazuri na yeye. Hivyo kwa mahusiano mazuri naye hutupatia kibali.

(LUKA 10:16 Ye yote atakayewasikiliza ninyi amenisikiliza mimi, naye awakataaye amenikataa. Lakini anikataaye mimi amemkataa yeye aliyenituma.)


VIZUIZI VYA  NGUVU ZA MUNGU NAFSINI MWETU

ITAENDELEA………………………………………….





Comments

Popular posts from this blog