WANAWAKE WALIPWA KWA KUNYONYESHA



Wakina mama katika maeneo matatu ya Derbyshire,South Yorkshire ambapo kiwango cha unyonyehsaji kiko chini kati ya asilimia 21 mpaka 29 waliahidiwa kulipwa mpaka pauni 200.
Kati ya wanawake 108 walio katika mpango huu,wanawake 37 sawa na asilimia 34 tayari wamelipwa katika kipindi cha wiki sita mpaka nane.
Wakosoaji wakiwemo madaktari wanasema mradi huu unachochea uwepo wa vitendo vya rushwa.
Mpango mwingine utafuata ambao utakua mkubwa zaidi utakaowahusisha wanawake 4,000
Tayari Wanawake 58 wamejiandikisha.
Nchini Uingereza, asilimia 51 ya wanawake kwa kipindi cha wiki sita mpaka nane, scotland kwa asilimia 38.
Takwimu ziko chini zaidi kwenye maeneo yaliyo masikini mpka kwa kiasi cha asilimia 12.
Wataalamu wa afya wanasema watoto wanatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita, ili kuwalinda watoto dhidi ya maradhi.
Halikadhalika tafiti zinasema kuwa kunyonyesha mtoto kunamuepusha mzazi kupata maradhi ya saratani ya matiti na Ovari.
lakini hali haiko hivyo nchini Uingereza ikilinganishwa na nchi nyingine, asilimia moja tu ya watoto nchini humo hunyonya maziwa ya mama zao kwa miezi sita.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA