KIEMBA ATUA RASMI AZAM FC
- Ametua Azam kwa mkopo wa miezi sita akitokea Simba.
Amri Kiemba (kulia) akiwa katika mazoezi yake ya kwanza klabuni hapo jana jumatatu.
BENCHI la Ufundi la Azam FC chini ya kocha mkuu, Mcameroon Joseph Omog pamoja na wachezaji, wamemkaribisha kwa shangwe kiungo Amri Kiemba ambaye kwa mara ya kwanza alianza mazoezi na kikosi hicho jana Jumatatu.
Kiemba ambaye amesajiliwa kwa mkopo na Azam kwa muda wa miezi sita akitokea Simba, alianza mazoezi hayo sambamba na mchezaji mwingine mpya Muivory Coast, Sanaly Bamba ambaye ni kiungo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Omog alisema: “Nimefurahi kuona Kiemba tupo naye kwenye timu, ndiyo ameanza mazoezi leo lakini namjua ni mchezaji mzuri nimemfuatilia kwa kipindi kirefu.
“Nilimwona pia kwenye mechi ya Taifa Stars waliyocheza na Benin ni mzuri, ukweli najivunia kuwa naye.”
Kwa upande wa wachezaji, nahodha msaidizi wa Azam, Himid Mao alisema: “Kiemba ni mchezaji mzuri kila mtu anajua na hiyo ndiyo sababu viongozi wakamleta kwenye timu. “Ninachoweza kusema, kama wachezaji tutampa ushirikiano mzuri tufanye kazi kwa ajili ya maendeleo ya timu.
Katika mazoezi hayo hawakuwapo wachezaji walio katika timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’. Hao ni Mwadini Ally, Abdallah Heri na Khamis Mcha.
DOMAYO, BOKO WATUA SAUZI
Wachezaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, Frank Domayo na Joseph Kimwaga wapo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya majeraha yao.
Bocco ambaye ni mshambuliaji, anasumbulia na maumivu ya goti, Domayo ambaye ni kiungo ana matatizo ya msuli wa paja wakati Kimwaga anaumwa goti, naye ni mshambuliaji.
Daktari wa Azam FC, Mbaraka Twalib amesema: “Wachezaji hao, wamekwenda kwa ajili ya vipimo vya juu ili kufahamu maendeleo yao baada ya kufanyiwa matibabu.”
Mshambuliaji Kelvin Friday aliyekuwa mgonjwa pia naye ameanza mazoezi.

Wachezaji kutoka nje ya nchi aliyefika ni Mrundi Didier Kavumbagu pekee.
DOMAYO, BOKO WATUA SAUZI
Wachezaji wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’, Frank Domayo na Joseph Kimwaga wapo Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya majeraha yao.
Bocco ambaye ni mshambuliaji, anasumbulia na maumivu ya goti, Domayo ambaye ni kiungo ana matatizo ya msuli wa paja wakati Kimwaga anaumwa goti, naye ni mshambuliaji.
Daktari wa Azam FC, Mbaraka Twalib amesema: “Wachezaji hao, wamekwenda kwa ajili ya vipimo vya juu ili kufahamu maendeleo yao baada ya kufanyiwa matibabu.”
Mshambuliaji Kelvin Friday aliyekuwa mgonjwa pia naye ameanza mazoezi.
Comments
Post a Comment