ASKARI WA FFU APIGWA JIWE ANG'OLEWA MENO SITA
Pc Idd Makame(25) akiwa wodini
Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwadui uliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung’olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo (kwa lugha ya Kisukuma Nh'ago) na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Novemba 21,2014 saa mbili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth iinayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa kampuni ya ulinzi ya Zenneth Security Services Limited inayolinda mgodi huo ilipata taarifa kuwa kuna wachimbaji haramu maarufu kwa jina la Wabeshi waliotaka kuvamia mgodi huku wakiwa na silaha za jadi ikiwemo mishale,mikuki,virungu,makombeo,mapanga na fimbo.
Comments
Post a Comment