IKULU YAHUSISHWA NA ESCROW
Ikulu
Bunge la Tanzania hapo jana liliambiwa kwamba afisa mmoja wa ikulu ya rais bwana Prosper Mbena aliandika barua ili kushinikiza hatua ya kutolewa kwa billioni 306 fedha za Escrow kutoka banki kuu ya Tanzania.
Bwana Mbena ambaye anafanya kazi kama katibu katika afisi ya rais aliandika barua mwaka uliopita akiiagiza wizara ya fedha kuzitoa fedha hizo kama ilivyoamrishwa na mwanasheria mkuu.
Kushirikishwa kwa ikulu ya ya rais kulizuka baada ya wabunge kujadili ripoti kuhusu kashfa hiyo ambayo imeikumba serikali ya Tanzania katika miezi kadhaa iliopita.
Kiongozi wa upinzani katika bunge,Bwana Freeman Mbowe pamoja na kinara wa bunge upande wa upinzani bwana Tandu Lissu alifichua jukumu lililochukuliwa na afisa huyo wa ikulu kushinikiza madai kwamba baadhi ya maafisa wakuu serikalini walihusika katika utoaji wa mabilioni hayo ya fedha.
Ripoti hiyo imesema kuwa fedha hizo za Escrow ni za walipa ushuru wa Tanzania na kwamba zilitolewa kwa njia ya ufisadi na kugawanywa miongoni mwa watu maarufu.
Chanzo cha habari BBC
Comments
Post a Comment