OBAMA AHIIDI KUSHIRIKIANA NA REPUBLICAN



Kiongozi mpya wa Baraza la Senate la Marekani kutoka chama cha Republican na Rais Barack Obama wote wameahidi kumaliza mvutano wa kisiasa ambao umewavunja moyo wapiga kura wa Marekani.
Wanachama wa Republican wamepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi wa nusu muhula na kwa sasa wanadhibiti mabunge yote mawili nchini Marekani.
Kiongozi wa baraza la Senate anayeingia madarakani Mitch McConnell amesema ataliwezesha baraza hilo kufanya kazi na kupitisha miswada ya sheria.
Bwana Obama amesema alikuwa na "hamu ya kufanyakazi na baraza jipya la Congress na kufanya miaka miwili yake aliyobaki kukaa madarakani kuwa na tija kadiri iwezekanavyo".




Senata Mitch McConnell kiongozi wa Republican katika Baraza la Senate, akipunga mkono na mke wake.
Kampeni za uchaguzi zilitawaliwa na kukata tamaa kwa wapiga kura kuhusu baraza la Congress kushindwa kufanyakazi pamoja.
Kwa Wamarekani waliopiga kura ya kutaka mabadiliko "nimewasikia."amesema Rais Obama.
Amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani kuwa pande zote mbili lazima zishughulikie matatizo hayo, lakini amekiri kama rais ana wajibu wa kipekee kujaribu kuona chombo hiki kinafanya kazi".
Rais Obama ataandaa mkutano wa viongozi wa Democrat na Republican Ikulu siku ya Ijumaa.
"Kwa kweli tunaweza kupata njia za kutuwezesha kufanyakazi pamoja," Bwana Obama amesema. "Ni wakati kwetu kushughulikia masuala ya manufaa kwa umma."


Wananchi wa Marekani wakipiga kura katika uchaguzi wa katikati ya muhula Novemba 4,2014
Lakini ameonya kuwa atachukua uamuzi binafsi kupunguza uondoaji wa wageni na kuimarisha usalama wa mipaka-hatua ambayo aliichelewesha hadi baada ya uchaguzi, kitu kilichowachukiza sana baadhi ya wapiga kura wa Amerika ya Kusini.
Mapema Jumatano, Bwana McConnell aliahidi kulifanya baraza la Senate kuwa na tija zaidi.
"Baraza la Senate kwa miaka michache iliyopita, kimsingi halikufanya chochote," amesema. "Tunakwenda kufanya kazi na kwa kweli kupitisha sheria."
Pia ameapa "kufanyakazi pamoja" na Bwana Obama katika masuala ambayo wanaweza kukubaliana, kama vile mikataba ya kibiashara na marekebisho ya kodi.
Rajesh Mirchandani anaeleza kile ambacho matokeo hayo yana maanisha kwa urais wa Obama. Kufanyakazi katika mfumo wa vyama viwili vya siasa, hakumaanishi "tuishi katika mgogoro", amesema.
Pia Jumatano, mwenyekiti wa kamati ya taifa ya chama cha Republican ameita ushindi wa Republican katika uchaguzi wa katikati ya muhula "kukataliwa moja kwa moja kwa agenda ya Obama".
Reince Priebus amewaambia waandishi wa habari kuwa "Wamarekani hawataki sera za Barack Obama,"

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA