SOMO LA LEO JUMATANO TAREHE 2/11/2016 " HOFU "


           
1.Hofu ni roho kamili ambayo anaitumia shetani kututoa kwenye imani na kututenga na Mungu. Hofu husababisha Mungu kujitenga nasi kwa maana mwenye hofu hana imani na asiye na imani hana Mungu. Kwa maana nyingine hofu hutufanya tuwe chukizo kwa Mungu .
(EBRANIA 10:38-39
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. 
39 Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.)
2.  Hofu inatukosesha kibali cha kufanyika wana wa Mungu. Kwa maana mtu unapokuwa na roho ya hofu Roho wa Mungu anakuwa hayupo ndani yake
(RUMI 8:14-15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.)
3.Hofu ni dhambi kama dhambi nyingine .
Mtu  mwenye hofu hana tofauti na mtenda dhambi yeyote kwa maana hofu pia ni dhambi kama dhambi nyingine
(UFUNUO 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili. )
     4. Hofu huzuia kumiliki
Hofu hutukosesha kile ambacho Mungu ameweka kwa ijili yetu , ikiwa ni sehemu ya kazi biashara au mahali popote pale, kwa mfano mtu msomi anawezaona ni fedheha kufanya kazi isiyo ya aina yake kwa kuhofia watu kumcheka au kumdharau bila kujua kuwa pengine huko ndio mwanzo wa kufikia kusudi ambalo Mungu amemkusudia au ndio mwanzo wa kuvuka kwake na kuendelea mbele
(YOSHUA 1:9-11 9 Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako. 
10 Ndipo Yoshua akawaamuru maakida wa watu, akisema, 
11 Piteni katikati ya matuo, mkawaamuru hao watu, mkisema, Fanyeni tayari vyakula; kwa maana baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani, ili kuingia na kuimiliki nchi awapayo Bwana, Mungu wenu, mpate kuimiliki. )
    4.Hofu huleta kujidharau mwenyewe, na kuzuia kusudi la Mungu
(HESABU 13:1-3  Kisha Bwana akanena na Musa, akamwambia,
2  Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao.
3  Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na Bwana; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli.  17  Musa akawapeleka ili waipeleleze nchi ya Kanaani, akawaambia, Pandeni sasa katika Negebu mkapande milimani,
18  mkaitazame nchi ni ya namna gani; na watu wanaokaa ndani yake, kwamba ni hodari au dhaifu, kwamba ni wachache au wengi;
19  na nchi wanayoikaa kwamba ni njema au mbaya; kwamba wanakaa katika matuo au katika ngome;
20  nayo nchi ni ya namna gani, kwamba ni nchi ya unono au ya njaa, kwamba ina msitu au sivyo. Iweni na moyo mkuu, mkayalete matunda ya nchi. Basi wakati ule ulikuwa wakati wa kuiva zabibu za kwanza. 31  Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.
32  Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.
33  Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

Musa alipotumwa na Mungu aliwachagua wale watu aliowaona ni watu walio vichwa kumbe watu hao ndani mwao wao wenyewe walijiona ni wadogo kama panzi, hivi ndivyo pia watu tunazima makusudi ya Mungu ndani yetu kwa ajili ya roho ya hofu inayotufanya tujishushe wenyewe na kujiona hatufai, hali hii imesababisha kutokumvunia Mungu kwa kuhofia kuchekwa kudharauliwa au vile vile kuona hatuwezi kama mtu Fulani.



 (1SAMWELI 17:41-54 Huyo Mfilisti naye akamsogelea Daudi na kumkaribia; na mtu yule aliyemchukulia ngao yake akamtangulia. 
42 Hata Mfilisti alipotazama huku na huku, akamwona Daudi akamdharau; kwa kuwa ni kijana tu mwekundu, tena ana sura nzuri. 
43 Mfilisti akamwambia Daudi, Je! Mimi ni mbwa hata umenijia kwa fimbo? Mfilisti akamlaani Daudi kwa miungu yake.
44 Mfilisti akamwambia Daudi, Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni. 
45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana. 
46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli. 
47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu. 
48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. 
49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi. 
50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake. 
51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia. 
52 Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka ufikapo Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni. 
53 Kisha wana wa Israeli wakarudi kutoka katika kuwafukuza Wafilisti, wakateka nyara marago yao. 
54 Naye Daudi akakitwaa kichwa chake yule Mfilisti na kukileta Yerusalemu; lakini silaha zake akaziweka hemani mwake. )
Daudi alimshinda Goliati kwa kuwa aliishinda hofu ndani yake hakuangalia udogo wake wala ukubwa wa Goliati aliangalia Mungu aliye ndani yake na kufanikiwa kumuua Goliati

5.    Hofu huzima sauti ya Roho Mtakatifu ndani yetu
WARUMI 8:9 (REJEA BIBLIA YAKO)

KWA UFUPI 

NA MWALIMU PRISCA MWANG'OMBOLA 


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI