Posts

Showing posts from November, 2016

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

Image
NA MWALIMU PRISCA MWANG'OMBOLA  Nguvu za Mungu  hukaa kwa mtu anaye fanya maombi, huwezi kukaa  na nguvu za  Mungu kama wewe sio muombaji  maana ndio silaha kubwa ya  kuweza  kuzishinda hila za mwovu, kwa maana vita yetu haipo katika nyama na damu ipo katika roho na falme za wakuu wa giza.  Unapokuwa na nguvu za Mungu unakuwa na unakuwa na faida zifuatazo       1.  Unakuwa na uwezo wa kushinda nguvu za giza Nguvu za Mungu zinatupa kushinda nguvu zote za giza,  hivyo ni vyema kuhakikisha unatembea na nguvu za Mungu na kujilinda na Mambo yote yanayosababisha nguvu za Mungu kupungua au kuisha kabisa. (EFESO 6:10-13 10   Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.   11   Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.   12   Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu w...

RATIBA YA MAZISHI YA SPIKA WA BUNGE MSTAAFU MH . S. SITTA HII HAPA

Image
                                     Mwili wa aliyekuwa spika wa bunge,  Samuel Sitta unatarajia kuwasili nchini siku ya Alhamis ukitokea nchini Ujerumani ambapo alipokuwa akipatiwa matibabu. Taarifa hiyo imetolewa na Gerald Mongela ambaye ni msemaji wa familia.   Amesema mara baada ya mwili huo kuwasili nchini utapelekwa nyumbani kwa marehemu Masaki jijini Dar es Salaam na siku ya Ijumaa shughuli za kuaga zitafanyika katika viwanja vya Karimjee kisha kupelekwa bungeni mjini Dodoma. “Mwili wa mpendwa wetu mheshimiwa Samuel Sitta utawasili na ndege ya Emirates siku ya Alhamis saa tisa na nusu alasiri na baada ya hapo mwili tutauleta hapa nyumbani kwaajili ya kukaa nao na kupumzika kusubiri ratiba ya Ijumaa,” alisema Mongela. Mazishi ya Marehemu Samwel John Sitta yatafanyika siku ya Jumamosi Urambo mkoani Tabora.

MAREKANI :TRUMP AONGOZA KWA KURA, HAYA HAPA MAJIMBO ALIYOSHINDA MPAKA SASA

Image
Mgombea wa Republican, Donald Trump ameonekana kuongoza kwa mbali katika uchaguzi wa Urais wa Marekani unaoendelea huku majimbo muhimu yakiwa yameshapiga kura. Hillary Clinton alianza vizuri katika uchaguzi huo akiongoza lakini mambo yamebadilika na ndoto yake ya kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa taifa kubwa zaidi duniani imeanza kufifia. Trump ameshinda majimbo muhimu yakiwemo Ohio, Carolina Kaskazini na Florida, na sasa yamebaki majimbo 270 ya uchaguzi (electoral votes) na ana nafasi kubwa ya kuingia Ikulu. Hadi saa tatu usubuhi hii, Trump anaongoza kwa 244 dhidi ya 215 ya Clinton, na anasubiri kupata point 26 kufikisha 270 ambazo zitampa uhakika wa kuwa Rais mpya wa Marekani.

TANZIA: WAZIRI WA ELIMU WA ZAMANI JOSEPH MUNGAI AFARIKI DUNIA

Image
                   Joseph Mungai  Aliyewahi kuwa Waziri wa Elimu na Mbunge wa Mufindi, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.   Aidha mwanasiasa huyo mkongwe nchini alikihama chama chake cha CCM na kujiunga na chama cha siasa cha CHADEMA katika harakati za uchaguzi mkuu mwaka 2015. Joseph James Mungai alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1943

TANZIA: SPIKA WA BUNGE MSTAAFU MH SAMWELI SITTA AFARIKI DUNIA

Image
Tunasikitika kuwataarifu kuwa mzee wetu mpendwa S.Sitta amefariki dunia akiwa nchini  Ujerumani saa 7:50 muda wa Ujerumani. Mh Saweli Sitta alikuwa nchini Ujerumani kwa ajili ta matibabu

ATIMIZA NDOTO YAKE YA MUDA MREFU YA KUKAA KWENYE JENEZA KUPATA UZOEFU WA KIFO

Image
Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo Imetokea *Brazil* na Mwanamke mwenyewe anaitwa *Vera Lucia da Silva* na umri wake ni *miaka 44* ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza. Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote. *Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika alhamis  ya November  3 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.* Ndugu zake walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho. Mmiliki wa eneo la kuzikia liitwalo *Eternal Garden Funeral home*, *Paulo Araujo, aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote,* kama mgeni maalumu.* *Wakati akiwa ndan...

ATIMIZA NDOTO YAKE YA MUDA MREFU YA KUKAA KWENYE JENEZA KUPATA UZOEFU WA KIFO

Image
Mwanamke aliyekaa siku nzima kwenye Jeneza ili kupata uzoefu wa kifo Imetokea *Brazil* na Mwanamke mwenyewe anaitwa *Vera Lucia da Silva* na umri wake ni *miaka 44* ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza. Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote. *Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika alhamis  ya November  3 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.* Ndugu zake walipingana sana na wazo lake lakini baadae waliamua kukubaliana naye na kuvaa nguo nyeusi wakati walipomtembelea na kufanya kama wanatoa heshima za mwisho. Mmiliki wa eneo la kuzikia liitwalo *Eternal Garden Funeral home*, *Paulo Araujo, aliamua kumpa Jeneza Vera bila gharama zozote,* kama mgeni maalumu.* *Wakati akiwa ndani ya Jeneza mw...

SOMO LA LEO JUMATANO TAREHE 2/11/2016 " HOFU "

Image
            1.Hofu ni roho kamili ambayo anaitumia shetani kututoa kwenye imani na kututenga na Mungu. Hofu husababisha Mungu kujitenga nasi kwa maana mwenye hofu hana imani na asiye na imani hana Mungu. Kwa maana nyingine hofu hutufanya tuwe chukizo kwa Mungu . (EBRANIA 10:38-39 Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.   39   Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu . ) 2.  Hofu inatukosesha kibali cha kufanyika wana wa Mungu. Kwa maana mtu unapokuwa na roho ya hofu Roho wa Mungu anakuwa hayupo ndani yake (RUMI 8:14-15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. ) 3.Hofu ni dhambi kama dhambi nyingine . Mtu  mwenye hofu hana tofauti na mtenda dhambi yeyote kwa maana hofu pia ni dhambi kama dhambi nyingin...