MWAMUZI ALIYECHEZESHA SIMBA VS YANGA, SASA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA

Jonesia Rukyaa-Mwamuzi aliyechezesha pambano la Yanga vs Simba February 20, 2016
Jonesia Rukyaa-Mwamuzi aliyechezesha pambano la VPL Yanga vs Simba February 20, 2016
Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake  wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu.
Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka nchi ya Afrika ya Kati.
Imetolewa na shirikisho la soka Tanzania (TFF)

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA