Posts

Showing posts from May, 2025

MWANAUME ALIYEOA WAKE 27 SIKU MOJA AISHANGAZA DUNIA

Image
Fela Kuti: Mwanamuziki Mshujaa Aliyeoa Wake 27 kwa Siku Moja na Kuandika Historia ya Afrika Katika historia ya muziki wa Afrika, jina la Fela Anikulapo Kuti linang’aa kama mwanga wa matumaini na mapambano. Alikuwa siyo tu mwanamuziki mashuhuri kutoka Nigeria, bali pia mwanaharakati shujaa, aliyeitumia sanaa yake kupinga mfumo wa kisiasa, ukoloni mamboleo, na ukandamizaji wa haki za wananchi barani Afrika. Lakini mbali na ujasiri wake kisiasa, Fela pia aligonga vichwa vya habari duniani kote mwaka 1978, kwa tukio ambalo hadi leo linaendelea kuwashangaza wengi. Katika mwaka huo, Fela aliushangaza ulimwengu kwa kuoa wake 27 kwa siku moja – jambo ambalo halijawahi kufanywa na msanii yeyote wa Kiafrika wa wakati wake. Hafla hiyo ya kipekee haikufanyika kwa siri, bali ilihudhuriwa na viongozi wa kimila 12, ambao walialikwa rasmi kufungisha ndoa hizo kwa mujibu wa mila na desturi za Yoruba – kabila kubwa alilotoka Fela. Kilichofanya tukio hilo kuwa la kipekee zaidi ni kwamba wanawake wote 27 ...

KIMBUNGA DIKELEDI KUIKARIBIA TANZANIA, WAKAZI WA MAENEO HAYA WAPEWA TAHADHALI

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa rasmi kuhusu kimbunga Dikeledi kinachopitia Bahari ya Hindi karibu na pwani ya Msumbiji. Kwa mujibu wa tathmini ya hali ya hewa iliyofanywa, kimbunga hicho hakina athari za moja kwa moja kwa upande wa Tanzania, lakini kinaweza kuleta vipindi vya mvua kubwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara. TMA imeeleza kuwa kimbunga Dikeledi, ambacho kwa sasa kipo mwambao wa Msumbiji, kinatarajiwa kurejea katika Rasi ya Msumbiji leo alasiri. Ingawa hakitathiri moja kwa moja maeneo ya Tanzania, ukaribu wake na pwani ya kusini unatoa uwezekano mdogo wa kuibuka kwa mvua kubwa na upepo mkali. Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, vipindi vya upepo mkali na mawimbi makubwa ya bahari vinatarajiwa kuathiri ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi kati ya Januari 14 na 15, 2025. Hali hii inaweza kuwa changamoto kwa shughuli za uvuvi na usafirishaji wa majini, hivyo basi watumiaji wa bahari wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa kipindi hiki. TMA ilianza kutoa tahadhari...

TAHADHALI: MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA HII

Image
Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania TMA imetoa taarifa kuhusu utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, hali ya mawingu kiasi, mvua nyingi na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Mara, Morogoro na Manyara. Pia maeneo ya Kilimanjaro, Tabora, Kigoma, Katavyi, Lindi, Mtwara na Pwani yatapokea mvua nyingi na ngurumo za radi. TMA imetoa angalizo la mvua kubwa katika maeneo machache nchini Tanzania. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Mtwara,Lindi, Ruvuma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro. Maeneo Yafuatayo Magharibi mwa nchi mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora vipindi vifupi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache kwanzia leo jioni vinatarajiwa. Pia Kanda ya kati Mikoa ya Dodoma na Singida vipindi vifupi vya mvua nyepesi katika maeneo machache vinatar...

NAFASI ZA KAZI YA UHUDUMU WA NDEGE KUTOKA JOB JUNCTION TANZANIA

Image
EMPLOYER:Job Junction Tanzania LOCATION:Dar Es Salaam Minimum Education level: Bachelor JOB DESCRIPTIONS: * Provide information, guidance, and assistance for safety and comfort to passengers on board aircraft * Attend the “brief” and act on it * Conduct safety check before flight * Greet customers, check their tickets and accompany them to their seats * Prepare and serve drinks and food to passengers * Present emergency equipment and give instructions * Monitor and secure the cabin regularly * Comply with all aviation rules and regulations for safety and protection * Assist passengers and cabin crew during emergency situations * Provide special help to passengers with special needs (children, disabled persons, elders etc) * Submit analytic reports concerning flight incidents Requirements * Fluency in English, multilingual is preferred * MS Office knowledge * Customer service-oriented * Professional image * Excellent communication and presentation skills * Problem solving skills and abi...