Skip to main content

WALiOFUKIWA NA KIFUSI GEITA WAOKOLEWA





Wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuokolewa
Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano ya wiki iliyopita ambapo jitihada za kuwaokoa zilikuwa zikifanyika kwa takriban siku 4 mfululizo mhadi siku ya jana ambapo waokoaji walifanikiwa kucharanga mwamba na kupata upenyo uliowezesha mawasiliano kati ya waokoaji, na watu hao.
Zoezi limekamilika leo majira ya saa 5:02 asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.
Zoezi hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga.
Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, watu pamoja na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo walionekana kulipuka kwa shangwe na kuwapokea wahimbaji hao ambao kati yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa walikuwa wamajawa na hofu wakiamini kuwa wasahaulika.
Awali kabla ya kuokolewa, yalifanyika mawasiliano ya kuwatumia ujumbe kwa kutumia waya ili waseme wako wangapi na majina yao, ambapo walisema kuwa wako 15 na kwamba walikuwa na njaa na walihitaji maji, soda, uji n.k
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha zoezi la uokoaji lilivyokuwa ambapo watu hao akiwemo raia wa China wamepatiwa huduma ya kwanza na kisha kupelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.
Taarifa zaidi zitakujia kadri zinavyotufikia.





Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA

MAGONJWA 27 YANAYOTIBIWA NA ASALI YENYE MDALASINI