Posts

Showing posts from January, 2017

FARU FAUSTA: NDIO FARU MZEE KULIKO WOTE DUNIANI

Image
FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54 Ndio faru mzee duniani,sasa haoni .Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54. Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo. Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.

WALiOFUKIWA NA KIFUSI GEITA WAOKOLEWA

Image
Wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuokolewa Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano ya wiki iliyopita ambapo jitihada za kuwaokoa zilikuwa zikifanyika kwa takriban siku 4 mfululizo mhadi siku ya jana ambapo waokoaji walifanikiwa kucharanga mwamba na kupata upenyo uliowezesha mawasiliano kati ya waokoaji, na watu hao. Zoezi limekamilika leo majira ya saa 5:02 asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga. Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, watu pamoja na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo walionekana kulipuka kwa shangwe na kuwapokea wahimbaji hao ambao kati yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa walikuwa wamajawa na hofu wakiamini kuwa wasahaulika. Awali kabla ya kuokolewa, yalifanyika mawasiliano ya kuwatumia uju...