Posts

Showing posts from 2017

UAMUZI WA KAMATI YA UTENDAJI TFF KUHUSU ATAKAYEKAIMU NAFASI YA MALINZI KWA SASA

Image
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, iliyokutana jana  Jumamosi Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa shirikisho. Kadhalika, Kamati hiyo ya Utendaji ya TFF, imempitisha Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF. Viongozi hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakavyoamua kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine.  Kamati ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo. WAPITISHWA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI TWFA Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu mkoani Morogoro. Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa,...

MAJINA YA WAUAJI KIBITI HAYA HAPA , WAANZA KUSAKWA NCHI NZIMA

Image
                          

KAULI ZA MAWAKILI BAADA YA MALINZI NA MWESIGWA KUNYIMWA DHAMANA

Image
Baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwanyima dhamana Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na afisa wa fedha Nsiande Mwanga, jopo la mawakili wa utetezi wameonekana kutoridhika na wateja wao kukosa dhamana. “Washtakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani halafu wanaomba tena upelelezi wa kesi wakati suala tayari lipo mahakamani hiyo ndio pointi kubwa ambayo tumeiibua halafu kitu kingine tulichokiibua ni pamoja na maombi ya dhamana,”  Jarome Msemwa-wakili upande wa utetezi. “Tumeiomba mahaka itoe dhamana kwa wateja wetu, kuna sheria ya Bunge inayokataza dhamana halafu kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana. Kwa hiyo kwa amri ya mahakama ambayo imesomwa leo (jana) wateja wetu wanapelekwa rumande hadi Jumatatu Julai 3, 2017.” “Sikutarajia katika muda na wakati kama huu kutakuwa na mashitaka yanayowakabili yanayofika 28 ya aina ileile lakini ndani yake yanatengenezwa machache kufanywa ya tutakatisha fedha wakati mash...

FARU FAUSTA: NDIO FARU MZEE KULIKO WOTE DUNIANI

Image
FARU FAUSTA WA NGORONGORO ATIMIZA MIAKA 54 Ndio faru mzee duniani,sasa haoni .Ngorongoro yampa ulinzi wa kijeshi FARU Fausta ndio anayesadikiwa kuwa na umri mkubwa kuliko Faru wote duniani,mwaka huu amefikisha umri wa miaka 54. Faru Fausta yupo katika mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,lakini kutokana na uzee wake huo,sasa anakabiliwa na tatizo la macho la kutoona. Kufuatia hatua hiyo,uongozi wa Ngorongoro sasa umemuweka katika makazi maalum ndani ya hifadhi hiyo. Hatua ya mamlaka kuchukua hatua ya kumpa ulinzi maalum Faru Fausta inahofia kushambuliwa na wanyama wengine wakali na hususani fisi na Simba.

WALiOFUKIWA NA KIFUSI GEITA WAOKOLEWA

Image
Wakipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuokolewa Tukio hilo lilitokea siku ya Jumatano ya wiki iliyopita ambapo jitihada za kuwaokoa zilikuwa zikifanyika kwa takriban siku 4 mfululizo mhadi siku ya jana ambapo waokoaji walifanikiwa kucharanga mwamba na kupata upenyo uliowezesha mawasiliano kati ya waokoaji, na watu hao. Zoezi limekamilika leo majira ya saa 5:02 asubuhi na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Zoezi hilo limeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja na Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyuga. Mara baada ya zoezi hilo kukamilika, watu pamoja na wanahabari waliokuwepo katika eneo hilo walionekana kulipuka kwa shangwe na kuwapokea wahimbaji hao ambao kati yao walikuwemo wenye uwezo wa kuongea ambao walisimulia tukio lilivyokuwa pamoja na kusema kuwa walikuwa wamajawa na hofu wakiamini kuwa wasahaulika. Awali kabla ya kuokolewa, yalifanyika mawasiliano ya kuwatumia uju...