N'GWANA MALUNDI MTU WA UMBILE LA AJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KWENYE JAMII YA WASUKUMA
HEBU LEO MJUE VIZURI HUYU MTU WA MIUJIZA AITWAE NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza....