KIPRE TCHETCHE KURUDI AZAM

STRAIKA wa Azam FC, Kipre Tchetche, hayupo na kikosi chake, lakini uongozi wa klabu hiyo, kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Nassor Idrissa, umefafanua kwamba amekwenda kwao Ivory Coast kwa sababu ya matatizo ya kifamilia na leo Jumatatu atarudi nchini.
Tchetche mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, hakuwa na kikosi hicho kwa takribani wiki moja ambapo awali ilidaiwa aliondoka nchini bila kuaga uongozi wake.
Lakini Idrissa alisema: “Tunamtarajia Tchetche kesho (leo Jumatatu) atatua na ndege akitokea kwao Ivory Coast.
“Ameahidi mwenyewe kurudi na kilichomwondosha ni matatizo ya kifamilia ya kwao huko, lakini aliaga.”
Wachezaji wa kigeni,Mhaiti Leonel Saint- Preux na Mmali Ismail Diara wako nje ya uwanja kwa sababu ni majeruhi.
Diara anasumbuliwa na goti lakulia na ataendelea kukaa nje ya uwanja kama wiki mbili zijazo wakati Leonel aliumia enka ya mguu wa kulia, yeye anatarajiwa kuanza mazoezi wiki hii.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA