MBWA WAKUTWA WAKISHAMBULIA MABAKI YA MWILI WA BINADAMU.



 Mabaki ya mwili yaliyokutwa katika eneo la kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani Ruvuma yakikusanywa na wataaramu kutoka hospital ya mkoa wa Ruvuma

         MIFUPA ya masalia ya binadamu  wa jinsia ya kiume  ambaye hakuwezakufahamika  jina na kukadiliwa kuwa na miaka (30) yamegundulika na Zaujia Pilly (70) mkazi wa kijiji cha Lupapila wilaya ya songea mkoani Ruvuma  wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji baada ya kuwaona mbwa wakishambulia sehemu za mabaki hayo. Kamanda wa polisi mkoa wa  Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea oktoba 26 mwaka huu majira ya saa 9:45  alasiri  huko katika kijiji cha Lupapila mtaa wa Mahinya kata ya Subira nje kidogo ya manispaa ya Songea.

         Alisema kuwa  inadaiwa siku hiyo ya tukio kwenye msitu wa uwanja wa ndege ilikutwa mifupa ya binadamu  wa jinsia ya kiume  ikiwemo fuvu la Kichwa, Mbavu, Mikono na Miguu wakati sehemu ya kiuno na mapaja ikiwa imeharibika vibaya. Alifafanua kuwa mabaki ya mwili huo yaligunduliwa na Zaujia Pilly wakati akienda kuchimba dawa za kienyeji kwenye msitu huo ghafla aliwaona Mbwa wakifukuzana kugombania mabaki ya mwili wa binadamu. 
         
       Alieleza zaidi kuwa  Zaujia baada ya kugundua tukio hilo alitoataarifa katika uongozi wa serikali ya Mtaa na kisha taarifa zilipelekwa katika kituo kikuu cha polisi cha songea mjini ambako baadaye polisi walifika eneo la tukio wakiwa wameongozana na Daktari kutoka hospitgali ya Mkoa wa Ruvuma ambaye aliyafanyia uchunguzi mabaki ya mwili huo na kubaini kuwa  marehemu alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani kwenye eneo la kisogo kilichopelekea kifo chake.
Kamanda Msikhela alisema kuwa  kufuatia tukio hilo hakuna mtu yeyote anayehusishwa na jeshi la polisi mkoani Ruvuma linaendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho.


Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA