JAJA ACHEZA DAKIKA 352 BILA BAO
Genilson Santos ‘Jaja’
KIKOSI cha Yanga kimeondoka jana alfajiri kwenda Shinyanga kucheza Stand United wikiendi hii huku kikiwa na straika wake Genilson Santos ‘Jaja’ ambaye hajafunga hata bao moja katika dakika 352 alizoichezea timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.
Yanga imecheza mechi nne ambazo zote Jaja amecheza kwa dakika tofauti ambapo katika mechi tatu za kwanza alicheza dakika 90 na kufanya jumla ya dakika 270 pia akacheza dakika 82 dhidi ya Simba wikiendi iliyopita.
Jaja ambaye nyota yake iling’aa alipoifunga Azam FC mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-0 wa Yanga katika mchezo wa Ngao ya Hisani, alitoka bila kufunga alipocheza dhidi ya Mtibwa Sugar na timu yake kuambulia kipigo cha mabao 2-0.
Baada ya mechi hiyo, Yanga ilipata ushindi mara mbili mfululizo dhidi ya Prisons na JKT Ruvu kwa kuzifunga mabao 2-1 timu hizo kila moja lakini bado Jaja hakuweza kufunga bao na hata alipocheza dakika 82 dhidi ya Simba raia huyo wa Brazil hakuweza kuzifumania nyavu.

Hadi sasa Yanga imefunga mabao manne ambayo yamefungwa na wachezaji wanne ambao kila mmoja amefunga bao moja, hao ni kiungo Haruna Niyonzima, viungo washambuliaji Simon Msuva, Andrey Coutinho na beki Kelvin Yondani.
Akizungumzia ubutu wa Jaja, Kocha wa Yanga, Marcio Maximo alisema licha ya kutofunga, Jaja ni msaada mkubwa katika kikosi chake ambapo kitendo cha kuchungwa na mabeki zaidi ya wawili kimerahisisha kupatikana nafasi kwa wachezaji wengine ambao wameifungia Yanga mpaka sasa.
“Ukiangalia Jaja siku zote anachungwa na mabeki kwa nguvu zote kuna wakati utaona mabeki wawili wanamchunga kwa nguvu na kutoa nafasi kwa wengine ambao wanaifungia Yanga,” alisema Maximo.
Comments
Post a Comment