MWANAFUNZI ANUSURIKA KUTEKWA
Denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni (mwenye sare za shule) aliyenusurika kutekwa na njemba inayotambuliwa kwa jina moja la Omar.
HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
HALI bado tete! Polisi wa Kituo cha Magomeni jijini Dar, wamemkamata baba mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Omar baada ya kupokea kipigo ‘hevi’ kutoka kwa raia wenye hasira kali akihusishwa na utekaji wa denti wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere iliyopo maeneo hayo.
Tukio hilo lililokusanya kadamnasi lilijiri wikiendi iliyopita,Magomeni-Kagera, Dar wakati mwanafunzi huyo
akitokea shuleni.Kwa mujibu wa mashuhuda, denti huyo alipofika eneo hilo, baba huyo alimsalimia na baada ya kujibiwa salamu yake alianza kumchombeza kwa maneno matamu-tamu.
Baadhi ya raia wenye hasira kali waliotoa kipigo ‘hevi’ kwa Bw. Omar wakiwa wametanda eneo la tukio.
Makamanda wa Polisi waliofika eneo la tukio kumuokoa mtuhumiwa.
Njemba huyo alivuka mipaka na kumshika mkono na kutaka kumvutia ndani ya gari lililokuwa karibu yake ndipo Laila alipoamua kupiga mayowe ya kuomba msaada na hatimaye kuokolewa na wasamaria wema waliokuwa wakipita njia.”
Mtuhumiwa (Omar) akiwa ndani ya gari mara baada ya kipigo.
Mwanafunzi huyo aliendelea kusema: “Alianza kunifuatilia tangu kule, akanisalimia hujambo nikamjibu sijambo, akaniambia tena kwenu hawajambo, nikamjibu hawajambo, akaendelea kuniambia eti, nimfuate akanipe lambalamba, mimi nikakataa kwa
mama alinikataza kukubali kupewa lifti na vitu vingine kutoka kwa watu nisiowajua tangu aliposikia habari za watoto kutekwa na Noah nyeusi.
Wasamaria wema wakimuokoa mtoto huyo.
“Kila kitu nilimkatalia lakini yeye akawa anaendelea kuniambia maneno yake na kuanza kunivuta ndipo nikaona sasa naenda kufa hivyo ikanibidi nipige kelele ndiyo watu wakatokea na kumkamata kisha kuanza kumpiga mpaka walipofika polisi.”
Mmoja wa wasamaria wema akimuingiza binti huyo kwenye gari kumuondoa eneo la tukio.
Gazeti hili lilizungumza na mtuhumiwa aliyekuwa amehifadhiwa ndani ya gari, alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo alimuomba paparazi wetu kabla ya yote kwanza amuokoe na kifo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.
Binti akiwa kwenye gari mara baada ya kuokolewa.
“Chondechonde ndugu yangu, naomba kwanza mnilindie usalama wangu, hao jamaa wanataka kuniua bila sababu, mimi wala sikuwa na nia mbaya na huyo binti wananizushia tu, nilikuwa namsalimia tu,” alisema Omar kupitia upenyo mdogo wa juu ya dirisha la gari alilohifadhiwa.
Imeandaliwa: Richard Bukos, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
Imeandaliwa: Richard Bukos, Deogratius Mongela na Chande Abdallah.
Comments
Post a Comment