KIEMBA , KISIGA KITI MOTO

SARE tano za mfululizo zimewavuruga viongozi wa Simba ambapo juzi Jumamosi baada ya mechi yao na Prisons, viongozi hao wakiongozwa na Rais wao Evans Aveva, waliitisha kikao cha dharura na moja ya ajenda yao ilikuwa ni kujua nini tatizo kuanzia kwenye benchi lao la ufundi.
Katika hatua hiyo imeelezwa kuwa kocha Patrick Phiri na msaidizi wake, Seleman Matola wamepewa mechi tatu timu ibadilike.Kamati ya utendaji ya Simba imefanya pia uamuzi mgumu baada ya kukukubaliana kwa kauli moja kuwaondoa kambini Amri Kiemba,Shabaan Kisiga na Haroun Chanongo kwa madai kwamba inachunguza mwenendo wao na wakiridhisha watawarudisha.
Habari za ndani zinasema kwamba kamati hiyo ambayo jana ilikaa kikao na kocha ilijadiliana nae mambo mengi na wakakubaliana kuchukua uamuzi huo. Lakini Kocha Patrick Phiri baada ya mchezo wa juzi alisema: “Nitakaa na Amri Kiemba ili nizungumze naye na kujua tatizo lake ni nini mpaka acheze chini ya kiwango lakini katika mechi ijayo sitaweza kumtumia.”
Mmoja wa viongozi wa Simba, aliliambia Mwanaspoti kuwa uamuzi wao umetokana na timu yao kupata sare za mfululizo huku kukiwepo na taarifa za baadhi ya viongozi na wachezaji kuihujumu timu hiyo.
Chanzo hicho kilisema kuwa katika kikao kilichofanyika mara baada ya mechi yao na Prisons iliyochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya na kulazimisha sare ya bao 1-1, kilifikia makubaliano kwamba mabadiliko hayo yafanyike kabla ya mechi yao na Mtibwa Sugar itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.
Mabadiliko hayo yameamuliwa ikiwa ni wiki moja baada ya kuwepo taarifa kwamba Rais Aveva amefanya mabadiliko katika nafasi ya wajumbe wa Kamati ya Mashindano inayoongozwa na Mwenyekiti Mohamed Nassoro na tayari mjumbe mmoja Mohamed Omary amepigwa chini.
Hivyo mpaka sasa kamati hiyo imebaki na viongozi wanne ambao ni Mwenyekiti Nassoro na Makamu wake Idd Kajuna na wajumbe wengine wawili Hussein Simba na Gerry Yambi.
“Unajua kuna mambo ya kuhujumiana ndani ya timu, mabadiliko haya hayatakuwa kwenye benchi la ufundi tu bali hata upande wa wachezaji tutakaowaacha wakati wa dirisha dogo ambao wengine wanahujumu timu na wengine viwango vyao vimeshuka,” alisema kiongozi huyo.
Simba imecheza mechi tano na kutoka sare mechi zote na hivyo kuambulia pointi tano tu matokeo ambayo si mazuri kwao kwani inashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakati Prisons wao wanashika nafasi ya 10.
Aveva alishuhudia sare hiyo akiwa na baadhi ya wajumbe wake wa kamati ya Utendaji, Collin Frish, Said Tully, Mwenyekiti wa kamati ya mashindano Mohamed Nassoro na makamu wake Idd Kajuna ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji.
Phiri na KiembaPhiri juzi Jumamosi alijikuta aking’aka kwamba kiungo wake Amri Kiemba ndiye aliyechangia kuigharimu timu. Katika mchezo huo, Simba ndiyo ilikuwa ya kwanza kuandika bao dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji wake Mganda Emanuel Okwi hata hivyo mshambuliaji wa Prisons Hamis Maingo aliisawazishia timu yake bao dakika ya 89. Mechi hiyo ilichezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya
               Amri Kiemba

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA