Posts
Showing posts from June, 2017
KAULI ZA MAWAKILI BAADA YA MALINZI NA MWESIGWA KUNYIMWA DHAMANA
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwanyima dhamana Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na afisa wa fedha Nsiande Mwanga, jopo la mawakili wa utetezi wameonekana kutoridhika na wateja wao kukosa dhamana. “Washtakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani halafu wanaomba tena upelelezi wa kesi wakati suala tayari lipo mahakamani hiyo ndio pointi kubwa ambayo tumeiibua halafu kitu kingine tulichokiibua ni pamoja na maombi ya dhamana,” Jarome Msemwa-wakili upande wa utetezi. “Tumeiomba mahaka itoe dhamana kwa wateja wetu, kuna sheria ya Bunge inayokataza dhamana halafu kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana. Kwa hiyo kwa amri ya mahakama ambayo imesomwa leo (jana) wateja wetu wanapelekwa rumande hadi Jumatatu Julai 3, 2017.” “Sikutarajia katika muda na wakati kama huu kutakuwa na mashitaka yanayowakabili yanayofika 28 ya aina ileile lakini ndani yake yanatengenezwa machache kufanywa ya tutakatisha fedha wakati mash...