Posts

Showing posts from September, 2016

BARAZA KUU LA CUF LAMFUTA UANACHAMA PROF LIPUMBA

Image
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba. Taarifa kutoka katika mkutano chama hicho unaeleza kuwa, wajumbe wote waliohudhuria wamepiga kura ya kuridhia kufukuzwa uanachama kwa Prof. Lipumba. Hatua hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu Prof. Lipumba kurejea na kusema kuwa yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c).

MTANGAZAJI WA CLOUDS TV ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA WILAYA

Image
    Hudson Stanley Kamoga   mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv  Leo Septemba 10, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo. Miongoni mwa Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa, yumo pia mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tv kinachorushwa kila siku kuanzia jumatatu hadi Ijumaa. Hudson Stanley Kamoga ameteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara. Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kuteua watangazaji kushika nyadhifa mbalimbali kwani alimteua aliyekuwa Mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni. Wakurugenzi wengine walioteuliwa leo ni pamoja na;- Mwailwa Smith Pangani – Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Godfrey Sanga – Halmashauri ya Wilaya ya Mkal...

TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LAIKUMBA MWANZA NA KAGERA

Image
Mchana wa  leo Mikoa ya Kanda imekumbwa na tetemeko la ardhi ambapo nyumba kadhaa zimebomoka na inadaiwa kuna vifo kadhaa