MTOTO WA AJABU AZALIWA DODOMA,SURA NUSU MTU NUSU CHURA
Mkazi wa kijiji cha Chibwechangula Behelo wilaya ya Mpwapwa mkoani hapa, Ruth Stanely Matonya (26), amejifungua mtoto wa ajabu wa jinsia ya kike mwenye kichwa nusu.
Mtoto huyo ambaye alikuwa na sura inayofanana na ya chura huku viungo vingine vya mwili vikiwa vya binadamu, alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Tukio hilo limetokea jana katika kituo cha afya cha mtakatifu Luke kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa.
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Edwin Kihura, mama huyo baada ya kufika kituoni hapo alikuwa na uchungu mkali ambao uliendelea bila kukoma huku akisindwa kujifungua hali iliyosababisha afanyiwe upasuaji.
“Pamoja na uchungu huo mkali lakini hakuweza kijifungua kwa njia ya kawaida ingawa njia ilionyesha ipo wazi mtoto aweze kutoka tuliamua kumfanyia upasuaji ili kuokoa maisha ya mama huyu,” alisema Dk. Kihura.
Dk.Kihura alisema maendeleo ya ujauzito wake alipokuwa akifika kliniki yalikuwa hayaonyeshi mkao wa mtoto huyo na mapigo ya moyo yalikuwa hayapatikani .
“Miezi ya mwisho mama huyu alipokuwa akihudhuria kliniki tulikuwa hatupati mkao wa mtoto na mapigo ya moyo yalikuwa hayapatikani lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni kitu ambacho kilikuwa kikiwashangaza sana waganga na wauguzi wa kituo hiki,”alisema Mganga huyo.
Alisema baada ya kufanyiwa upasuaji walitoa mtoto huyo, akiwa na sura isiyoeleweka inayofanana na chura na kichwa nusu.
Akizungumzia tatatizo hilo linasababishwa na nini, Mganga huyo, alisema kuna sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na mama kukosa baadhi ya madini mwilini na hivyo uumbaji wa mtoto kutokamilika.
“Unasababishwa na sababu za kibailogia ambazo ni kushidwa kugawanyika kwa kromozome na tatizo kama hili limewahi kutokea mara chache sana
katika hospitali nyingi lakini vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka kwa wingi siku hizi za karibuni na kitaalamu linajulikana kama ANECEPHALY,”alisema Mganga huyo.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni baadhi ya kina mama kutumia dawa za kienyeji ambazo ni kali wakati mimba zikiwa changa zinaweka sumu kwa mtoto tumboni.
Alisema hali ya mama huyo inaendelea vizuri katika kituo cha mtakatifu Luke ambako anaendelea kupatiwa matibabu.
SOURCE: NIPASHE
Comments
Post a Comment