Posts

Showing posts from October, 2014

MAGAZETI YA LEO

Image

LIPUMBA; CCM ING'OKE KWANZA RUZUKU BAADAE

Image
                       Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba Wakati Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akisema suala la ruzuku na viti maalumu ni changamoto kwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hicho si kipaumbele. “Tunachokitaka ni kuunganisha nguvu zetu ili kuhakikisha tunaing’oa CCM madarakani kwanza, masuala mengine kuhusu ruzuku tutaweka utaratibu maalumu baadaye,” alisema. Profesa Lipumba ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema hayo Dar es Salaam jana alipokuwa akiwaeleza waandishi wa habari maazimio ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF lililokutana Jumatatu na Jumanne iliyopita. “Wenzetu Kenya waliweza kuungana na kuhakikisha wanaking’oa chama tawala madarakani, lakini sasa kwa hapa mkiungana na kuwa chama kimoja ni lazima msajili chama chenu, sasa tunachokitaka ni kushirikiana tu kwanza,’’ alisema. Alisema suala la ruzuku na uteuzi wa viti maalumu siyo lengo kuu la Ukawa i

BREAKING NEWS: AJALI NYINGINE KAHAMA USIKU HUU, DEREVA WA FUSO AFARIKI PAPO HAPO

Image
Inasemekana dereva wa semi hiyo amefariki huku dereva aliyekuwa akiendesha Coster akivunjika mguu baada ya magari haya kugoganga usiku huu katika eneo la Trans Oil Wilayani kahama katika barabara kuu iendayo nchi jirani za Burundi, Rwanda na Uganda. Endelea kufuatilia blog ya nyumbani kwa taarifa Zaidi.

AJALI MBAYA DARAJA LA WAMI LEO

Image
Basi aina ya Simba mtoto linalofanya safari zake Dar na Tanga limegongana uso kwa uso na Roli katikati ya Daraja la Wami ambapo dereva wa Roli amepoteza maisha papo hapo. Kwa taarifa zaidi tutazidi kukufahamisha.

PAZI AKAMILISHA MPANGO WA KASEJA KUTUA SIMBA

Image
                                                          Juma Kaseja KOCHA wa zamani wa Makipa wa Simba, Idd Pazi, amesema sasa ni muda mwafaka kwa kipa, Juma Kaseja, kurejea kwenye kikosi cha klabu yake hiyo ya zamani kutokana na uzoefu mkubwa alionao. Hivi karibuni kumekuwapo na taarifa za Kaseja kurejeshwa kwenye kikosi cha Simba ili akasaidiane na kipa chipukizi, Peter Manyika Jr pamoja na Hussein Shariff ‘Casillas’ kwani Ivo Mapunda anahusishwa na mpango wa kutemwa kikosini hapo. Pazi ambaye hivi karibuni aliondolewa kuinoa Simba baada ya klabu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za Ligi Kuu Bara, alisema Kaseja anaweza kuisaidia klabu hiyo lakini ameutaka uongozi wa kutatua matatizo mengine yanayochangia klabu hiyo kufanya vibaya. “Kaseja ni kipa mzoefu, ataisaidia Simba hivyo siyo jambo baya kumrejesha, pia amekuwa na historia nzuri na klabu hiyo kwa muda wa miaka 10 aliyokuwa pale,” alisema. “Hii pia itamsaidia Manyika ambaye ndiyo kwanza a

TAMBWE AIKARIBIA YANGA

Image
              Ammis Tambwe MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Amissi Tambwe, kwa sasa anaonekana si lolote katika timu yake ya Simba ambapo amefunga bao moja tangu msimu huu uanze, lakini imebainika kuwa mfumo anaotumia kocha wao Patrick Phiri ndio chanzo cha kuporomoka kwa straika huyo. Mchezaji huyo ambaye ameanza kuwatamanisha baadhi ya viongozi wa usajili wa Yanga, ametamka kwamba anamalizia mechi zake mbili zilizobaki Simba kufunga mwaka halafu arudi kwao Burundi ambako anaweza kufanya uamuzi mgumu kutokana na vitisho alivyopata klabuni kwake hivi karibuni. Habari za ndani zinadai Tambwe ambaye amebakiza miezi mitano katika mkataba wake ameanza kujadiliwa na baadhi ya vigogo wa Yanga ambayo tayari ina wachezaji watano wa kigeni, lakini mtihani ni jinsi ya kumshawishi kocha Mbrazili Marcio Maximo. Hata hivyo mabosi hao wanadai watajua cha kufanya baada ya kumaliza mechi zilizosalia mwaka huu na kusikia tathmini ya Kocha. Wakati Simba ilipokuwa chini ya

MTOTO WA DARASA LA TANO APEWA UJAUZITO

Image
Mtoto anayejulikana kwa jina la Paulina (14) alitundikwa mimba na mawanafunzi mwenzake. Mama mzazi wa Paulina, Luciana John ‘Mama Paulina’ (kushoto) akiwa na mwanaye huyo. Mtoto mmoja aliyejulikana kwa jina la Paulina (14) mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Boko, jijini Dar amekatisha masomo kutokana na kupata ujauzito. Akizungumza kwa huzuni huku akilia, mtoto huyo alisema kwa sasa haendi shuleni kutokana na kuwa na ujauzito wa miezi miwili alioupata kwa kijana aliyemtaja kwa jina moja la Paulo mkazi wa Mbweni ambaye ni mwanafunzi wa sekondari. Alisema: “Paulo alikuwa rafiki wa kaka yangu na alikuwa akija sana nyumbani kwetu, tukawa tumezoeana sana na siku moja akanishawishi twende kwao, tukaenda na huko ndiyo tukafanya mapenzi baada ya kuniambia atanioa nikimaliza shule. “Alikuwa akinipa fedha mara nyingine elfu mbili au tatu ambazo nilikuwa nikizitumia shuleni, mwishowe ndiyo nikanasa,” alisema Paulina. Akizungumza kwa huzuni mama wa mtoto h

WEMA NA DIAMOND WAACHANA

Image
Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.              Staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.          BMW la   Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’. Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. KUMBE NI MUDA MREFU TU Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa. SAFARI YA CHINA Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wann

BUNGE LA BURKINA FASO LACHOMWA MOTO

Image
Waandamanaji wakilitazama bunge la Burkina Faso likiteketea kwa moto. Waandamanaji hao wakishangilia baada ya kuchoma bunge.…                              Magari nayo yameteketezwa kwa moto. WAANDAMANAJI nchini Burkina Faso leo wamechoma moto bunge la nchi hiyo kupinga kupitishwa kwa katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongeza muda wa kukaa madarakani. Rais Compaore anataka kuongeza muda zaidi katika utawala wake wa miaka 27 aliyotumia kuliongoza taifa hilo. Taarifa kutoka Mji Kuu ya nchi hiyo, Ouagadougou, zinasema kuwa ukumbi wa chama tawala na makao makuu ya chama hicho cha Congress for Democracy and Progress yamechomwa moto pia. Bunge hilo lilitaka kubadili katiba itakayomuwezesha Compaore, aliyeingia madarakani tangu mwaka 1987 ili aweze kuiongoza tena nchi hiyo mwakani. Kumekuwepo kampeni za wapinzani wanaomtaka rais huyo kuachia ngazi na kutogombea katika uchaguzi wa mwaka ujao. Kabla ya kuchomwa moto bunge hilo, polisi walilipua m

TIM COOK WA KAMPUNI YA APPLE ASEMA ANAJIVUNIA KUWA SHOGA

Image
                                   Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook. MTENDAJI Mkuu wa kampuni ya Apple ya Marekani, Tim Cook, amefichua kwamba yeye ni shoga na anaona fahari kuwa hivyo. Cook ameyasema hayo leo katika tahariri ya mtandao wa Businessweek.com kwamba: “Acha niseme wazi. Ninaona fahari kuwa shoga, na ninaona kuwa shoga ni moja ya zawadi kubwa zaidi ambazo Mungu amenipa.” Ameongeza kusema kwamba wafanyakazi “wengi” wa Apple wanafahamu kwamba yeye ni shoga na haoni tofauti yoyote kuhusu wanavyoshirikiana naye. Cook anakiri kwamba jambo la kufichua hali hiyo halikuwa rahisi, lakini alifanya hivyo kwa kutaka jamii imwone yuko sawa na watu wengine. “Sijioni kuwa mwanaharakati katika jambo hili, bali ninatambua nilivyonufaika katika kujitoa mhanga kwa wengine. Hivyo, iwapo kusikia kwamba mkuu wa Apple ni shoga kunaweza kumsaidia mtu fulani kuelewana na wengine, au kumfariji mtu yeyote anayejihisi kuwa mpweke, au kumtia moyo mtu apiganie usawa katika jamii, basi ku

UGOMVI WASABABISHA AMUANDALIE MUMEWE MIPIRA YA KIUME KAMA CHAKULA

Image
Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya Kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha kati yao. Mwanamke huyo ambaye ni mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya "Trust" kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari. Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, mwanamke huyo aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa muda kabla ya kuvikaanga kwa mafuta ya kupikia na viungo vingine. Wakati mumewe alipowasili kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira hiyo kama mboga na nyingine ikiwa na mkaa. Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti. Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume huyo amb

MAGAZETI YA LEO

Image