WAISLAMU WAHISI KUONEWA NA SERIKALI, NI KUTOKANA NA ASKOFU GWAJIMA KUACHIWA KWA DHAMANA WAKATI SHEHE PONDA AMENYIMWA DHAMANA HADI LEO
SIKU
chache kupita baada ya Mkutano wa 19 wa Bunge kumalizika,na serikali
kuutupia mbali mswaada wa sheria ambao unaruhusu kuwepo makakama ya
Kadhi nchini kutajadiliwa kwenye mkutano huo,
Nayo Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini wameibuka na kutoa tamko
zito kwa kuwataka waislam wote nchini kutoshiriki kwenye kura ya maoni
ya kupitisha katiba pendekezwa Bunge Maalum la Katiba,kwa madai kwamba
serikali haina nia nzuri na waislam nchini kwa kitendo chake cha kukataa
kuwepo mahakama ya Kadhi nchini.
Vilevile Taasisi hiyo imewataka pia waislam wote kujitokeza
kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura na kujiandaa kufanya uamuzi
mgumu ambao wanasema hajawai fanywa na waislam nchini tangu taifa kupata
Uhuru.
Akisoma Tamko hilo lenye kura sita jana jioni kwenye msikiti
wa Kichangani uliopo Magomeni Jijini Dar es Salaam ,Naibu Katibu Mkuu
wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam nchini Sheikh Mussa Kundesha kwa niaba
ya asasi za kiislam 11 zinazounda umoja huo na kushuhudiwa na Mamia ya
waumini wa dini hiyo pamoja waandishi wa Habari ambapo Sheikh Kundesha
alisema-
Waislam wote nchini wamechoka na uonevu wanaodai kufanyiwa na
Serikali iliyoko madarakani kwa kitendo cha kuondo Mswaada wa Mahakama
ya kadhi Bungeni ambapo alisema ni kuendelea kuchochea vita ya kidini
nchini.
“Kuna kila sababu ya kuamini kuwa Serikali ya CCM imeshindwa
kulishughulikia suala la mahakama ya Kadhi katika uhalisia wake kama
ilivyoahidi kupitia ilani yake kwenye uchaguzi ibara ya 108 (b) mwaka
2005 na sasa inafanya hadaa za kisiasa kuwadanganya waislam ili
waonekane inalishughulikia suala la mahakama ya Kadhi kama walivyoahidi”
“Kwa ubabe huu wanaotufanyia waislam sasa tunawaomba waumini wote wa
kiislam nchini kutoipigia kura katiba pendekezwa kwasababu sio katiba
nzuri kwa waislam harafu tunawataka kila mmoja aliyetimiza miaka 18
ajiandikishe kwenye Daftari wa wapiga kura kujiandaa kufanya uamuzi
mgumu ambapo utalitikisa nchi”alisema Sheikh Kundesha.
Alisema kuwa kitendo cha Serikali kuwatambua Makadhi wa
Bakwata pamoja wanachosema ni ‘Mahakama hewa ya Kadhi’ chini ya Bakwata
ni kinyume na Katiba ya nchini ibara 19(1) na (20) kwa kuwalazimisha
waislam wawe chini ya Bakwata ambapo wanasema hawatakubaliana nalo.
KUHUSU TAMKO LA MAASKOFU.
Pia katika Tamko la Taasisi hiyo kiislam ambapo litasomwa kila
msikiti Ijumaa wiki hii nchi nzima pia wamezungumzia Matamko mawili
yaliyotolewa Jukwaa la kikiristo nchini ambapo Taasisi hiyo ya Kiislam
wameonyesha masikitiko yao kwa kusema ni dhahili hapa nchini kuna
serikali dhaifu kwa kuwaacha maaskofu kutoa matamko ambayo wanadai ni ya
kichochezi.
“Ushahidi kwamba ni chuki tu husda ni pale ambapo hata waislam
tuliopendekeza mahakama ya Kadi iwekwe kwenye Katiba pendekezwa,lakini
tunashangaa hawa maaskofu wamekuwa wakiipinga Mahakama hii wakati hii
dini tofauti na y a kwao na sisi waislam tumewavumilia lakini tunahoji
hawa maaskofu wanataka nini”
KUHUSU KESI ZA MASHEIKH NA KUNYIMWA DHAMANA.
Pia Taasisi ya Kiislam wameonyesha kuchukizwa kwa kitendo cha Masheikh
mbalimbali akiwemo shehe Ponda ambao wapo mahabusu na kunyimwa Dhamana
na Serikali ila wanashangaa kitendo cha Serikali kuwamwachia Askofu wa
Kanisa la Ufufuo na Uzima Askofu Josephat Gwajima wanadai kitendo hicho
kinaonesha Serikali kuwapendelea wakristo.
“Masheikh mbalimbali wako mahabusu wakinyimwa Dhamana bila sababu za
msingi kwa kesi za uchochezi au kwa kisingizio cha Ugaidi wakati huo huo
tumeshuhudia Maaskofu wakitoa kauli za uchochezi pasina kuchukuliwa
hatua yeyote ikiwemo sakata la Askofu Gwajima”
KAMPENI WANAO DAI KUUA MADRASA.
Pia Taasisi hiyo wamezungumia kitendo cha Serikali kuwakamata wa Mashehe
mbalimbali wanaowafundisha watoto majumbani kwa madai ya serikali
kutofuata taratibu za mafunzo likiwemo matukioa tofauti yaliyotokea
mkoani arusha-
Kwa kusema ni wazi serikali imejitosa kuua madrasa nchini.
“Lakini Takriban mwezi mmoja sasa,njama hizi za kuua madrasa zetu
zimeibuka kwa kasi kubwa na nguvu kwa kuendesha kamatakamata ya waalimu
wa madrasa zao katika hali duni majumbani mwao wakifundisha Quran na
mafunzo mengine ya Uislam kama tulivyoshudia huko mkoan Moshi na Arusha”
“Tunataka Serikali itusaidie kufundisha Elimu ya dini ya Kiislam kwa
mujibu wa sheria ndiyo ipi,sheria hiyo ilipitishwa lini na Bunge
lipi?kwa mujibu wa Katiba ya nchi ibara 20 (1) kazi ya kutangaza dini ni
suala binafsi,iweje sasa Serikali inakuja na madai haya ya kufundisha
dini kinyume na Sheria kwa walimu wetu wa madrasa”
Comments
Post a Comment