KAULI YA JOSE MOURINHO KUHUSU TUZO ZA BALON D'OR
Unaikumbuka kauli ya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger aliyoitoa kuhusu kupinga kutolewa kwa tuzo za mchezaji bora wa dunia za Ballon d’Or?
Kauli yake hiyo imeonekana kupewa uzito na sasa ni zamu ya kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye ameungana na kauli ya Wenger na kusema yupo sahihi na kwamba lengo la soka linabadilika kutoka timu za soka hadi kwa mchezaji binafsi.
Tuzo hiyo inaonekana kutawaliwa na wachezaji wawili Lionel Messi pamoja na Cristiano Ronaldo toka mwaka 2008 na mwaka huu tena imekwenda kwa Ronaldo ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo baada ya kufunga magoli 52 katika mechi 43 alizokuwa amecheza.
Comments
Post a Comment