MAJAMBAZI YAVAMIA GARI LA BONITE MOSHI, YAUWA DEREVA NA MLINZI NA KUPORA MAMILIONI
Mlinzi wa Kampuni ya Bonite, aliyetambulika kwa jina la Edson Shamba baada ya kupigwa risasi na majambazi mjini Moshi.
Dereva wa Kampuni ya Bonite aliyetambulika kwa jina la Amini Mselemu mara baada ya kushambuliwa kwa risasi na majambazi.
Tarehe 20/04/2015, majira ya saa 12 jioni, katika eneo la Soweto ya chini eneo la Radio Kli Fm, Kata ya Soweto, Tarafa ya Moshi Magharibi, Wilaya ya Moshi, gari la Bonite lenye usajili wa namba T.803 ATR aina ya Toyota Hiace lililotoka kwenye makusanyo ya fedha za mauzo lilivamiwa na majambazi wapatao wanne wakiwa na Bastola huku wakitumia usafiri wa pikipiki mbili aina ya Boxer na Srm.
Katika tukio hilo mtu aitwaye Edson Shamba(56), Mnyiramba mkazi wa matindigani ambaye alikua ni mlinzi na alikua akisindikiza gari hilo akiwa na bunduki aina ya Short Gun namba 8710653 ikiwa na risasi tano aliuwawa papo hapo kwa kupigwa risasi maeneo ya kichwa, ambapo Amini Mselemu(61), Mnyao, mkazi wa mtaa wa Chunya Moshi aliyekua dereva wa gari hiyo, alipigwa risasi maeneo ya kifuani, tumboni, mkononi na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu usiku wa jana katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo mjini Moshi.

Majambazi hao walipora fedha yote ya mauzo ambayo thamani yake bado haijajulikana na kisha kutokomea kusikojulikana.
Watu wanne ambao ni wakala wa mauzo wa kampuni hiyo wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano. Watu hao walikuwa ndani ya gari hilo wakati wa tukio.
Miili yote ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya rufaa ya KCMC mjini Moshi na jeshi la polisi linaendelea na kuwatafuta wahusika ili kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Imetolewa na :
G.Y. Kamwela-SACP,
Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Imetolewa na :
G.Y. Kamwela-SACP,
Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Comments
Post a Comment