WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU WAFUKIWA NA KIFUSI



Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika kijiji cha Karore,Kata ya Runguya,tarafa ya Msalala Wilaya ya  Kahama Mkoani Shinyanga. 
Kamanda wa polisi mkoani humo , JUSTUS KAMUGISHA   amesema kwa siku za karibuni wachimbaji hao wali acha  kuchimba kutokana na machimbo yalikuwa hayaonekani ,   lakini juzi kuna mchimbaji mmoja aliona kuna dalili za kuonekana kwa machimbo hayo na ndipo akawapigia wenz ake  simu kwa ajili ya  kwenda   kuanza shughuli za uchimbaji lakini ilivyofika jana shughuli hizo zilisitishwa.

Kwamujibu wa Kamanda KAMUGISHA,usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.

Amesema miili tayari imeshat olewa kutoka kwenye mashimo hayo,lakini  bado wanaendelea na juhudi za  kuangalia kama kuna miili  mingine imebakia.

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUKAA NA NGUVU ZA MUNGU SEHEMU YA KWANZA