SUGU ATOA MACHOZI BUNGENI KUHUSU MWANAYE, NAIBU SPIKA ADAI MJADALA UFUNGWE KULINDA HAKI ZA MTOTO
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amejikuta akiangua kilio bungeni baada ya kutoa hoja binafsi kumjibu Mbunge wa viti maalum wa Singida ‘CCM’ Martha Mlata, aliyemshutumu kwa kumpora mtoto wake wa kike Sasha kutoka kwa mzazi mwenzake Faiza Ally.
Akijibu tuhuma za Mlata, Sugu alisema kuwa ameumizwa na kusitikishwa kwa suala la kifamilia kuingizwa ndani ya bunge na kuomba kuheshimiwa kwa kuwa masuala yale ni masuala binafsi.
“Asante sana Naibu Spika, naomba nitoe maelezo binafsi, tarehe 25 June 2015, Mbunge Martha Mlata alidai kuwa kuna Mbunge wa CHADEMA amempora mwanamke mmoja mtoto mdogo wa miaka miwili na amempora wakati Mbunge huyo amekuwa hatoi matunzo kwa mama yake… Mlata aliwataka Wabunge wote wanawake kuungana kukemea kitendo alichodai kimefanywa na Mbunge huyo," Alisema Sugu na Kuongeza:
“Hakutaja jina la Mbunge aliyemhusisha na madai yake ila alidai kuwa ni msanii mwenzake… hata hivyo alitaja jina la mwanamke anayedaiwa kunyang’anywa mtoto kuwa ni Faiza. Mbunge aliyelengwa na mashambulizi ni mimi Joseph Osmond Mbilinyi, mimi ndiye baba wa mtoto Sasha Desderia Mbilinyi anaedaiwa kuporwa kwa mama yake, na Faiza aliyetajwa ni Faiza Abdallah Ally ambaye ni mzazi mwenzangu na mama mzazi wa Sasha Desderia.
“Watu wazima hawapendelei kuzungumzia mambo binafsi hadharani… Nadhani sitakosea kusema hata Mheshimiwa Martha mwenyewe asingependa kuzungumzia matatizo yaliyopelekea ndoa yake kuvunjika.
“Mimi ni mmoja wa watu wazima wenye akili timamu ndio maana sijazungumzia hadharani kuhusu uhusiano wangu na mzazi mwenzangu Faiza Ally na mtoto wetu Sasha… Sasha ameishi na mama yake tangu alipozaliwa mwaka 2012, katika kipindi chote nimempelekea mama yake laki tano kila mwezi, nimemlipia ada ya shule Milioni 3 kila mwaka.. Mlata kama angekuwa anataka kujua angeniuliza ningempatia taarifa hizi kabla hajarusha tuhuma nzito.
“Mwanamke anayedaiwa kuwa mnyonge anajulikana katika kumbi za starehe nchi nzima, picha zake zilisambazwa katika Mitandao ya Kijamii na kuleta fedheha kubwa kwa watu wanaojali maadili ya mavazi, picha zake nyingine akiwa amevaa diapers zilisambaa mitandaoni na Martha Mlata angeweza kupata ukweli wa mambo haya kabla hajarusha tuhuma mbele ya Bunge.
“Nilienda Mahakama ya Mwanzo Manzese, niliwasilisha ushahidi kwamba mzazi mwenzangu asingeweza kumlea mtoto.. Mahakama ilimwita akajitetea, June 23 Mahakama iliridhika na ushahidi wangu, ikaamua mtoto akabidhiwe kwangu ili nimlee.
"Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
"Kilichodaiwa kuwa ni uporaji wa mtoto kiukweli ni amri ya Mahakama, Mlata hakuwahi kuonekana Mahakamani, nina mashaka hata kama anamfahamu mtoto mwenyewe au mama anayemwita mwanamke mnyonge“
“Mashauri haya hayakupaswa kuwekwa hadharani kama alivyofanya Martha Mlata… Nimesikitishwa na Martha Mlata kuzungumza mambo binafsi.
"Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa”.
Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisimama na kuomba mjadala huo ufungwe ili kulinda haki za mtoto.
"Pamoja na Mahakama kunipa haki, mtoto bado yuko kwa mama yake kwa sababu mimi ni mstaarabu… nimetoa nafasi ili Majadiliano ya kifamilia yafanyike… Naomba mjadala huu usiendelee zaidi ya hapa”.
Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisimama na kuomba mjadala huo ufungwe ili kulinda haki za mtoto.
Comments
Post a Comment