Posts

Showing posts from December, 2014

IVO AGOMA KUKAA GOLINI

Image
                                                        Ivo Mapunda KIPA Ivo Mapunda ametangaza rasmi kwamba anaondoka Simba na amemtaka kocha wake, Patrick Phiri, asimpange tena katika mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara kwani amechoka kutuhumiwa kuwa anaihujumu timu. Ivo ametoa kauli hiyo baada ya mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 yeye akiwa langoni. Mashabiki wamemlalamikia kuwa alifungwa bao hilo kizembe. Ivo amesema  kuwa hataki tena kukaa langoni katika mechi za Simba za ligi na nyinginezo kwani imani ya mashabiki kwake imepotea kwani hata akifungwa katika mazingira ya kawaida haeleweki. “Nafanya kazi katika mazingira magumu mno, sina raha wala amani ndani ya timu, kila mechi nikidaka lazima nilaumiwe sasa kuna haja gani ya kuendelea kusimama langoni? Nitazungumza na kocha asinipange tena kudaka mechi zilizobaki, nataka nikae benchi,” alisema Ivo. Hii ina maana Simba itapaswa kumtumia kipa chipuki

MTOTO WA MIEZI MITATU AATHIRIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Image
                           Zena akiwa na mtoto wake Dar es Salaam. Mtoto mwenye umri wa miezi mitatu, mkazi wa Buza, Dar es Salaam amebainika kuwa mwathirika wa dawa za kulevya. Damu na mkojo vya mtoto huyo (jina tunalihifadhi) vilichukuliwa na kupimwa katika maabara ya Hospitali ya Mwananyamala na baada ya saa mbili, majibu yalitoka na kuthibitisha kwamba alikuwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroini. Taarifa za kitabibu zinaonyesha kuwa kuwapo kwa heroini mwilini mwa mtu, huweza kuonekana katika mkojo ndani ya siku mbili hadi nne iwapo dawa hizo zilitumiwa na mhusika kwa kati ya saa mbili hadi tano. Hatua ya kumfanyia vipimo mtoto huyo wa kiume, inatokana na jitihada za gazeti hili kutaka kufahamu jinsi utumiaji wa dawa za kulevya kwa wanawake wajawazito na wale wanaonyonyesha unavyoweza kumwathiri mtoto akiwa tumboni au anayenyonya maziwa ya mama mwathirika. Mtaalamu wa tiba katika Hospitali ya Mwananyamala, Dk Elifasi Mritu anasema: “Ni kweli ukit

WASHTAKIWA MAUAJI YA DK. MVUNGI WAZUA KIZAA KIZAA MAHAKAMANI

Image
Polisi wakiimarisha ulinzi Mahakamani  Dar es Salaam. Washtakiwa 11 wa kesi ya mauaji ya  kukusudia ya Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk.  Sengondo Mvungi wamegoma kushuka kizimbani  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakishinikiza kuelezwa jalada la kesi yao lipo wapi na imefikia katika hatua gani. Sakata hilo limetokea leo majira ya saa 4:00 asubuhi, muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kumueleza Hakimu Mkazi, Hellen Liwa kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine kwa kutajwa. Baada ya wakili Njike kueleza hayo, mshtakiwa Longishu  Losingo alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 16,2014 upande wa mashtaka uliwaambia jalada la kesi yao lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), leo (jana) wanatuletea hadithi, tunaomba watueleze uhalisia wa kesi hii, tupo gerezani tunateseka. Kwa upande wa mshtakiwa Masunga Makenza naye alidai kuwa yeye hafahamu sheria, kesi yao ni ya mud

UCHAWI: BIBI KIZEE AKUTWA KAANGUKA NJE YA KANISA ASUBUNI ALIPOKUWA AKIWANGA USIKU.

Image
Bibi kizee mmoja huko mkoani Mbeya ambae jina lake halikuweza kufaamika mara moja, amekutwa ameanguka nje ya kanisa akiwa uchi wa mnyama kwa kile kilichodaiwa alikuwa anawanga. Kikongwe huyo alionekana ni mwenye kuishiwa nguvu pia kuhema sana, alipozinduka alijikuta amezingirwa na watu asubuhi huku akiwa ni mwenye woga wa wingi wa watu hao. Katika kumuhoji haraka haraka alieleza kuwa alikuwa anasafiri safari zake za usiku kutokea mkoani Morogoro kuelekea Ruvuma na alipopita maeneo hayo ya kanisa alijikuta anavutwa na kitu asichokijua ndipo kukapelekea kuanguka kwake. Watu wa maeneo ya bibi huyo alipoanguka hawakuweza kumtambua na kuonekana hakuwa anaishi hapo ndipo walipomuuliza anakotoka na akajibu kuwa anatokea mkoani Morogoro na alikuwa anaenda Ruvuma kikazi yaani kazi zake za kishirikina. Tukio la wachawi kuanguka karibu na maeneo ya makanisa mkoa wa Mbeya hutokea mara kwa mara na hivi inajiidhirisha kuwa nguvu za giza zinazotawala maeneo mbalimbali mbele ya Mungu

NDEGE YA AIR ASIA YAPOTEA IKIWA NA ABIRIA 160

Image
Ndege ya AirAsia (QZ8501) imepotea leo hii ikiwa na watu zaidi ya 160 ikitokea Indonesia kwenda Singapore.  An Air Asia flight travelling from the Indonesian city of Surabaya to Singapore has lost contact with air traffic control, the company has said. Indonesian media say more than 160 people were on board the Airbus A320-200. The aircraft, flight number QZ8501, lost contact with air traffic control at 07:24 (00:24 GMT), Air Asia  tweeted .

IVO, MASHABIKI BIFU ZITO

Image
                         Kipa wa Simba, Ivo Mapunda. NI bifu! Ndiyo unavyoweza kusema baada ya mashabiki   wa Simba kumshushia lawama za moja kwa moja kipa wao namba moja, Ivo Mapunda kutokana na kipigo cha bao cha 1-0, walichopata kutoka kwa Kagera Sugar. Mchezo huo wa raundi ya nane, ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Baada ya mchezo huo, mashabiki walitoa lawama kwa Mapunda kuwa ndiye aliyechangia kufungisha bao hilo kutokana na kutokuwa makini langoni. “Wewe angalia mpira wa kurushwa baada ya kuupiga ngumi anataka kuudaka, kama siyo uzembe ni nini,” alisikika shabiki mmoja akilalamika.“Huyu Mapunda siku zote hawezi kucheza mipira ya krosi na hata bao lile limedhihirisha hilo, nashangaa kwa nini mpaka sasa ameshindwa kubadilika, bao lile ni uzembe wake,” alisikika shabiki mwingine. Lakini wakati mashabiki wakisema hivyo, kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri alitoa lawama zake kwa washambuliaji wake kwa madai kuwa walishindwa kutumia nafasi nyingi walizo

SIMBA YAMTELEKEZA KWIZERA DAR

Image
Kiungo  wa zamani wa Simba, Mrundi, Pierre Kwizera. KIUNGO  wa zamani wa Simba, Mrundi, Pierre Kwizera hivi sasa ana wakati mgumu hapa jijini Dar, kutokana na uongozi wa klabu hiyo kumtelekeza kwa kutomlipa madai yake, baada ya kumvunjia mkataba wake pamoja na mwenzake, Amissi Tambwe. Simba iliwavunjia mikataba nyota hao kutokana na kutoridhishwa na uwezo wao uwanjani na nafasi zao kuchukuliwa na Waganda, Simon Sserunkuma na Juuko Murushid.Habari zilizopatikana ni kwamba Simba wamevunja makubaliano ya malipo yao, ambapo ilitakiwa walipwe chao tangu Desemba 17, mwaka huu lakini uongozi wa klabu hiyo umeshindwa kufanya hivyo huku wakikataa hata kupokea simu zao. Mtoa habari alikwenda mbali na kusema kuwa kwa sasa Kwizera anatia huruma kutokana na kuwa na wakati mgumu ambapo Simba wamekuwa wakimpiga danadana kuhusu kupewa malipo yake ambayo ni dola 7000 (zaidi ya shilingi milioni 11). “Kwizera hivi sasa anaishi maisha magumu, hana pesa kabisa hata kula kwake siku hizi kumekuwa k

KATIBU YANGA ASAKWA NA POLISI

Image
Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu. JESHI  la Polisi jijini Dar es Salaam limekuwa likiendelea kumsaka aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu. Habari za kipolisi kutoka ndani ya Jeshi hilo zimeeleza kwamba juhudi za kumtia nguvuni Njovu anayetuhumiwa na ubadhilifu zimekuwa zikiendelea kwa juhudi kubwa. “Unajua askari wetu walikwenda kumshika Njovu wakiongozana na mwanasheria wa Yanga, lakini akashitukia mtego na kutimua mbio. Sasa juhudi zinafanyika ili kumshika kwa kuwa tuna RB yake. “Lengo ni kumtia nguvuni ili aweze kujibu mashitaka yanayomkabili kuhusiana na ubadhirifu,” alisema mtoa habari ambaye hakutaka kuandikwa gazetini kwa madai yeye si msemaji wa jeshi hilo.kwa upande wa Yanga, Mkurugenzi wa Habari, Jerry Muro alisema wanajua Jeshi la Polisi ndilo linahusika na suala la ufuatilia. “Sasa kama liko mikononi mwa polisi, basi tuwaachie wao, nafikiri haitakuwa vizuri sisi tukawa wasemaji tena. Watakapokamilisha mambo yao kwa kufuata taratibu zao, huenda wakaeleza kin

DUDE: WASANII WENGI WA BONGO WANA UKIMWI

Image
                   Kulwa Kikumba ''Dude'' Staa wa Fialmu za kibongo Kulwa Kikumba ''DUDE'' amesema kuelekea mwisho wa mwaka wasanii wengi wana UKIMWI na mbaya zaidi wanaambukizana wao kwa wao.  Dude amesema mastaa wazima wanahesabika na kutaja sababu kuwa ni kuibiana na kubadilishana wapenzi bila woga. “ Utakuta Mbongo Fleva ana mtu kwenye Bongo Muvi na Mbongo Muvi ana mtu kwenye dansi au kwa mamis au hata wacheza mpira, ukitaka kuujua ukweli tangaza dau kuwapima mastaa uone watakaojitokeza,” alisema Dude. Aidha, Dude alisema anavyoona yeye ingeanzishwa kampeni ya mastaa wa Bongo kupima Ukimwi kwani anawahofia watoto wa kizazi kipya zaidi ambao wanajikuta wanaingia pabaya na kuzima ndoto zao.  Chanzo Gazeti la Ijumaa

ROBERT HUTH: BEKI WA STOKE CITY ALIYEUSHANGAZA ULIMWENGU KWA KUICHUKIA CHRISTMAS

Image
Beki raia wa Ujerumani anayecheza kwenye klabu ya Stoke City Robert Huth hali imekuwa tofauti baada ya mchezaji huyo kuonyesha hisia za kinyume kabisa na wachezaji wengine . Mchezaji huyu aliustaajabisha ulimwengu kwa kitendo chake cha ku-tweet hisia zake kuhusiana na sikukuu hii ambayo inadhimishwa ulimwenguni kote. Robert Huth kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter aliandika kuwa anaichukia krismasi na hakutoa sababui za msingi za chuki aliyo nayo kwa sikukuu hii . Hakuna aliyeweza kufahamu chanzo hasa cha utofauti huu toka kwa beki huyu Mjerumani ambaye amejijengea sifa kama beki mgumu asiyetetereshwa na washambuliaji awapo uwanjani .

AFARIKI AKIJARIBU KUWARUSHIA BOMU WENZAKE

Kuna taarifa kuwa mtu mmoja amekufa wakati akijaribu kuwarushia wenzake bomu ambalo limemlipukia mwenyewe, leo usiku huko Mazengo, Songea. Chanzo cha kuwarushia bomu wenzake bado kujulikana, Uchunguzi bado unafanywa.

MAXIMO AONDOKA RASMI YANGA

Image
            Maximo Habari rasmi toka ndani ya klabu ya Yanga zinasema kuwa kocha Mbrazil Marcio Maximo ameondoka ndani ya klabu hiyo. Maximo anaondoka Yanga baada ya uongozi wa klabu hiyo kukubaliana naye kuvunja mkataba aada ya kushindwa kuelewana juu ya jinsi ya kuiendesha klabu hiyo kwenye masuala ya ufundi. Yanga ilishikilia msimamo wa kumuajiri Mkurugenzi wa ufundi ambaye alipangwa kuwa Charles Boniface Mkwasa jambo ambalo Maximo hakukubaliana nalo. Nafasi ya Maximo sasa itachukuliwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm ambaye aliifundisha timu hiyo kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Mholanzi mwenzie Ernst Brandts. Tukio hili linaendeleza historia ya Yanga kufukuza makocha baada ya kufungwa na Simba kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts msimu uliopita kufuatia kipigo cha 3-1 mbele ya Simba iliyokuwa inaongozwa na Dravko logarusic.

HOUSE GIRL ALIYEMPIGA MTOTO UGANDA AHUKUMIWA MIAKA MINNE JELA

Image
                      Jolly Tumuhiirwe Mahakama nchini Uganda imetoa hukumu ya miaka minne jela kwa mfanyakazi wa ndani, Jolly Tumuhiirwe, aliyepatikana na hatia ya kumtesa na kumpiga motto wa miezi 18. Tumuhiirwe, 22, alionekana kwenye video iliyosambaa mtandaoni akimpiga bila huruma mtoto huyo aitwaye Aneela. Msichana huyo aliwaomba radhi wazazi wa mtoto huyo na umma kwa ujumla na kudai kuwa hakujua nini kilimtokea hadi kutenda unyama huo.

KPAH SHERMAN NI JEMBE

Image
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Kpah Sherman (kulia) akiwa na meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam akitokea Cyprus jumatano  STRAIKA matata wa Liberia, Kpah Sean Sherman, ametua Yanga Jumatano mchana tayari kwa mapambano, lakini ametoa angalizo kwamba atafanya yake ndani ya mwaka mmoja kisha asepe. Mchezaji huyo aliyefunga mabao 24 kwenye Ligi Kuu Cyprus msimu uliopita, amewaambia viongozi wa Yanga kwamba hataki kufanya kazi muda mrefu Jangwani, ndiyo maana anataka mkataba mfupi. Akizungumza baada ya kuwasili, Sherman alisema amefurahi kujiunga na Yanga na anataka kutumia nafasi hiyo kukabiliana na changamoto mpya katika maisha yake. “Sijasaini mkataba wowote, lakini naamini kila kitu kitakuwa sawa baada ya kukutana na viongozi, nataka kupata changamoto mpya nikiwa hapa, sina wasiwasi na uwezo wa kutekeleza majukumu yangu uwanjani kwani ninaimudu vyema kazi yangu ya mshambuliaji,”alis

PHIRI: MAXIMO KAPATA

Image
                                 Maxio Maximo SAA chache baada ya kutua katika kikosi cha Yanga, straika Danny Mrwanda amepewa jezi namba 24 iliyokuwa ikivaliwa na kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ lakini mwenyewe ameikataa na anataka apewe namba 33. Kocha wa Simba, Patrick Phiri, aliposikia mchezaji huyo amesaini Jangwani akachanganyikiwa, lakini akafunguka ya moyoni. Katika siku yake ya kwanza ya mazoezi na kikosi cha Yanga juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Mrwanda alionekana amevaa jezi namba 24 na kuonyesha uwezo wake mbele ya Kocha Marcio Maximo. Meneja wa Yanga mwenye mamlaka ya ugawaji wa jezi na namba za wachezaji, Hafidh Saleh, alisema amempa Mrwanda jezi hiyo iliyokuwa ikivaliwa na Chuji, lakini ameikataa na sasa anajipanga kumpa jezi nyingine namba 33. “Nimempa Mrwanda jezi namba 24 ya Chuji ambayo haikuwa na mtu kwa sasa, lakini ameivaa kwa shingo upande na sasa haitaki anataka namba 33 ambayo tupo katika mchakato wa kumpatia,” alisema Hafidh.

IVO, MATOLA WAKUNJANA

Image
                    kipa wa Simba,Ivo Mapunda  HALI ya kambi ya Simba iliyopo kisiwani Unguja, Zanzibar si shwari baada ya Kocha Msaidizi, Seleman Matola na kipa Ivo Mapunda, kutaka kurushiana makonde baada ya kutofautiana kauli walipokuwa wakitafuta suluhu ya tofauti zao za muda mrefu. Habari kutoka kambini humo zinadai kuwa wawili hao juzi Jumanne walitofautiana kauli baada ya mazoezi ya asubuhi na kuzuka ugomvi ulioamuliwa na kocha Patrick Phiri kwa kuwataka wakae pembeni na kumalizana kiutu uzima, baadaye walisuluhishwa na mratibu wa kambi hiyo, Abdul Mshangama. Chanzo cha habari kiliendelea kusema kwamba ugomvi wa Matola na Mapunda ulianza tangu kipindi ambacho Mapunda aliumia kidole walipokuwa kambini wakijiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara na juzi Mapunda alishindwa kuuvumilia na kutaka suluhu. Imeelezwa kuwa Matola alikuwa akimshutumu pia Mapunda kuwa amekuwa akiruhusu mabao mepesi jambo linaloigharimu timu hiyo kitu ambacho Mapunda hakukubaliana nacho. Tuhuma hizo

KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

ALIYEWAKOSOA WATOTO WA OBAMA AJIUZULU

Image
                        Watoto wa Obama wakiwa na mama yao New York, MArekani. Wakati watanzania wametajwa kuhusika na kashfa ya wizi wa sh 306 bilioni katikaakaunti ya Tegeta escrow wakigoma kujiuzulu, mfanyakazi wa Repiblican,Elizabeth Lauten amejiuzulu baada ya kuwakosoa watoto wa rais Barack Obama. Elizabeth Lauten ambaye ni Ofisa Mkuu wa Mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher,alijiuzulu jana baada yab kushambuliwa na watu kadhaa kwa kuwakosoa watoto hao kwa kuvaa nguo fupi wakati wa hafla ya jioni iliyofanyika ikulu, Marekani. Lauten aliwataka watoto hao kuwa makini wanapokuwa katika matukio ambayo jamii inawatazama kupitia vyombo vya habari. Lauten, aliwakosoa Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook, lakini baada ya muda mfupi kupita alifuta ujimbe huo kutokana na watuwengi kumshambulia. Akiomba radhi Lauten alisema baada ya kutafakari aligundua kwamba hata yeye wakati mtoto hakupenda kukosolewa. "Baada ya maombi ya saa kadhaa am

MAGAZETI YA LEO DESEMBA 12

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .