Posts

MZAZI MWENZA WA JOSEPH MBILINYI (SUGU) APOROMOSHA MATUSI MTANDAONI

Image
Mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, mwanadada Faiza Ally ameamua kuwatolea uvivu watu wanaodai kuwa ameachwa na mheshimiwa huyo kutokana na mavazi yake.  Faiza ambae ana mtoto na Sugu, katika instagram ameandika:“Sasa leo ngoja nifunguke…. Yaani nikiweka picha zangu kwa raha zangu mnaanza kusema oh ndio maana SUGU kakimbia ndio maana kaniacha Nasema hivi MIMI NDIO NIMEMUACHA mkome kunisema nimeachana na nimemuacha tukiwa kwenye process za ndoa na tulishakutana na padri na kwenye jumuiya nilisha anza  Kuna vitu vikinifanya niondoke kabla ya ndoa ambavyo vitabaki kuwa vya kifamilia ……. Nyie mna muona sugu Kama si mtu wa kawaida mm namuona Kama alie kuwa mpenzi wangu na Sasa ni baba wa mtoto wangu …. Lkn anajua ubora wangu na faida zangu Pumbavu zenu nyote mnao zani niliachwa tena kwa mavazi anajua na anapenda mavazi yangu ….. Nachukia kuamka asubuhi na kukuta comments za kusemwa vibaya…. Nyie mnajua tabia zake ????? Au mnamuona kwa mbali ...

UWASILISHWAJI WA RIPORT YA PAC KUHUSU TEGETA ESCROW ACCOUNT

Image
Baada ya bunge kwenye kikao cha asubuhi kusema swala la Escrow limeingizwa kwenye ratiba na ripoti itawasilishwa kuanzia jioni ya leo .  Tujumuike kwa pamoja kuhabarishana yanayojiri jioni hii bungeni Dodoma kuhusu sakata la Escrow. Anaekalia kiti jioni hii ni spika mwenyewe mama Anna Makinda Katibu:  Bunge lipokee na kujadili ripoti maalumu Waziri wa sheria(Migiro):  Katiba ya jamuhuri imezingatia mgawanyo wa mihimili, kuna zuio la muda la mahakama, shauri hili la 2014 lilikua na nia bunge lisijadili ripoti, mahakama katika barua yake ilikusudia bunge liendelee shughuliki zake kama zilivyopangwa. Makinda:  Spika anatoa nasaha chache kabla hajaruhusu mjadala na Zitto anaitwa ZITTO:  Taarifa ina sehemu mbili na itasomwa na mwenyekiti na makamu mwenyekiti na anaanza kuisoma ripoti, Migogoro ilitakiwa iishe kwanza ili pesa zililipwe 2014 March kamati ya PAC ilikutana na BoT ili kujadili pesa zilizo kwenye walisema pesa zimeshatolewa na zimeshalipwa IPTL, kamati i...

KESI YA MSICHANA WA KAZI ZA NDANI UGANDA SASA YABADILISHWA NA KUWA JARIBIO LA KUTAKA KUUA

Image
Polisi wamebadilisha mashtaka ya mfanyikazi wa nyumbani aliyenaswa kwa kamera akimpiga na kumtendea unyama mtoto wa mwaka mmoja na nusu, kutoka kwa kosa la kutesa na sasa anakabiliwa na kosa la jaribio la mauaji. Video hiyo iliwaudhi watu wengi sana kwenye mitandao ya kijamii ila babake mtoto huyo alisema walisambaza video hiyo ili kuwatahadharisha wazazi wenegine. Mfanyakazi huyo wa nyumbani Jolly Tumuhirwe, alikuwa amezuiliwa katika gereza la Luzira na mahakama ya Nakawa kw a kosa la kutesa chini ya kifungo cha 41 kwenye katiba kinachoongelea dhidi ya mateso. Mwanamke huyo sasa anatarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 8 Disemba. Hata hivyo, msemaji wa polisi Bwana Fred Enanga, amesema "shtaka dhidi ya mwanamke huyo lilibadilishwa baada ya kupitiwa mwendesha mkuu wa mashitaka. Tumuhirwe alikubali kosa la kumpiga mtoto huyo kwa kurunzi, tuki olililonaswa kwa kamara ya CCTV. Polisi walimfanyia Tumuhirwe uchunguzi wa kiakili na kubaini kuwa ana akili timamu. Afisaa mkuu wa ...

ASKARI WA FFU APIGWA JIWE ANG'OLEWA MENO SITA

Image
Pc Idd  Makame(25) akiwa wodini Kumetokea tukio la aina yake katika mgodi wa madini ya almasi wa Mwadui uliopo katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambapo askari polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pc Idd  Makame(25) amejeruhiwa vibaya mdomoni kwa kung’olewa meno sita baada ya kupigwa jiwe kwa kutumia kombeo  (kwa lugha ya Kisukuma Nh'ago)  na watu wanaodaiwa kuwa ni wachimbaji haramu wa madini katika mgodi wa Mwadui wakati akitimiza wajibu wake wa kuhakikisha usalama wa raia na mali zao Tukio hilo la kusikitisha limetokea Novemba 21,2014 saa mbili na robo usiku katika eneo la Tanex katika mgodi huo wakati askari huyo akiwa na askari wenzake wakiongeza nguvu baada ya askari wa kampuni ya ulinzi ya Zenneth iinayolinda mgodi wa Mwadui kushindwa kuwadhibiti wachimbaji wadogo wa madini maarufu "Wabeshi" waliotaka kuingia kwa nguvu mgodini wakiwa na silaha za jadi. Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malun...

KIEMBA ATUA RASMI AZAM FC

Image
Ametua Azam kwa mkopo wa miezi sita akitokea Simba.   Amri Kiemba (kulia) akiwa katika mazoezi yake ya kwanza klabuni hapo jana jumatatu.  BENCHI la Ufundi la Azam FC chini ya kocha mkuu, Mcameroon Joseph Omog pamoja na wachezaji, wamemkaribisha kwa shangwe kiungo Amri Kiemba ambaye kwa mara ya kwanza alianza mazoezi na kikosi hicho jana Jumatatu. Kiemba ambaye amesajiliwa kwa mkopo na Azam kwa muda wa miezi sita akitokea Simba, alianza mazoezi hayo sambamba na mchezaji mwingine mpya Muivory Coast, Sanaly Bamba ambaye ni kiungo. Akizungumza na Mwanaspoti, Omog alisema: “Nimefurahi kuona Kiemba tupo naye kwenye timu, ndiyo ameanza mazoezi leo lakini namjua ni mchezaji mzuri nimemfuatilia kwa kipindi kirefu. “Nilimwona pia kwenye mechi ya Taifa Stars waliyocheza na Benin ni mzuri, ukweli najivunia kuwa naye.” Kwa upande wa wachezaji, nahodha msaidizi wa Azam, Himid Mao alisema: “Kiemba ni mchezaji mzuri kila mtu anajua na hiyo ndiyo sababu viongozi wak...

UTEKAJI NA MAUWAJI JIJINI DAR YAZIDI KUSHIKA KASI

Image
    Lile sakata la utekaji na mauaji ya watoto, sasa limechukua sura mpya na kulifanya Jiji la Dar kuwa mahali salama kwa kuishi kufuatia kutekwa na kuuawa kwa wasichana wawili na mfanyabiashara mmoja huku watoto wawili wakiwa hawajulikani walipo, Uwazi lina data za kutosha. Marehemu Jack enzi za uhai wake. Kwa nyakati tofauti, gazeti hili limewahi kuripoti mara kadhaa juu ya utekeji wa watoto wadogo hususan wanafunzi ambao baadaye hupatikana wakiwa wameuawa na baadhi yao wakikatwa viungo vyao nyeti hali inayoonesha kuwa ni mambo ya kishirikina. Lakini safari hii, inaonekana kuwepo mtandao wenye malengo maalum. WATOTO WAWILI WATEKWA, HAWAJAPATIKANA Watoto wawili ambao ni majirani wanaoishi Mbagala Kipati, Kuluthumu Selemani (14) na Aisha Muhidin (13), Novemba 10, mwaka huu walitoweka baada ya kuaga majumbani mwao wanakwenda madrasa kwa Ustaadh Hafidhi Sharahani Rashid, lakini tangu siku hiyo hawajaonekana tena. Kwa mujibu wa chanzo, siku chache kabla ya watoto ha...

YALIYOJIRI BUNGENI LEO

Image
Habari wakuu, Leo moja kwa moja kutoka bungeni, aliekalia kiti leo ni mheshimiwa mama Anna Makinda. Swali la kwanza linaulizwa na Freeman Mbowe na linahusu wizara ya afya. Swali : Serikali ina mkakati gani kuongeza watumishi (tasnia ya afya) (Lorensia Jeremia-Bukwimba) Jibu:  Walau jitihada inaonekana kwa allocation iliofanyika Swali:  Serikali ina mkakati gani kuongeza vitetendea kazi na vifaa tiba Jibu: Intergreted logic system itasaidia pia itakuja sheria ya kulazimisha watu kujiunga kwenye mifuko badala ya hiyari na mifuko italeta uwezo wa kununua vifaa tiba Swali:  Ukosefu wa wahudumu wa afya unapelekea wasio na ujuzi kuhudumu na wengi wanaondoka kwenda nchi nyingine (Suzan Lymo) Jibu:  Kimepatikana kibali cha kuajiri wahudumu wapya mwaka huu, mambo yanaenda vizuri japo malengo ya milenia yanaweza yasifikiwe, lakini serikali haina uwezo wa kuzuia watumishi kuhama nchi Swali:  Hospitali ya mkoa wa Mara inajengwa kwa kasi ndogo (Vincent Nyerere) Jibu: ...