TAHADHALI: MVUA KUBWA KUNYESHA MIKOA HII
Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania TMA imetoa taarifa kuhusu utabiri wa hali ya hewa nchini Tanzania. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, hali ya mawingu kiasi, mvua nyingi na ngurumo za radi vinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Dar es Salaam, Mara, Morogoro na Manyara.
Pia maeneo ya Kilimanjaro, Tabora, Kigoma, Katavyi, Lindi, Mtwara na Pwani yatapokea mvua nyingi na ngurumo za radi.
TMA imetoa angalizo la mvua kubwa katika maeneo machache nchini Tanzania. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa, vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo machache ya mikoa ya Mtwara,Lindi, Ruvuma na Kusini mwa mkoa wa Morogoro.
Maeneo Yafuatayo Magharibi mwa nchi mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora vipindi vifupi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache kwanzia leo jioni vinatarajiwa.
Pia Kanda ya kati Mikoa ya Dodoma na Singida vipindi vifupi vya mvua nyepesi katika maeneo machache vinatarajiwa
Aidha Nyanda za Juu Kusini Magharibi mikoa ya Rukwa Songwe, Mbeya, Njombe na Iranga. Mvua Kubwa inatarajiwa katika maeneo machache kwanzia kesho.
Pwani ya Kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): vipindi vifupi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo.
Kwa hiyo TMA imetangaza angalizo la mvua kubwa katika maeneo machache ya mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya Unguja.
Comments
Post a Comment