Kumekuwa na Maswali mengi miongoni mwa watu, kuhusu mikoa inayosemekana kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Baada ya kufuatilia vyanzo mbali mbali vya habari, na kufanya mlinganisho na maoni ya watu, mikoa iliyotajwa kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania nikama ifuatayo; Sumbawanga (Rukwa), Sumbawanga ni wilaya inayopakana katika mkoa wa Rukwa. Wilaya hii imekuwa maarufu kuliko hata mkoa wenyewe kulingana na historia, pamoja na matukio kadha wa kadha ya kishirikina yanayotokea katika wilaya hiyo. Uchawi maarufu unaotumika Sumbawanga huwa ni uchawi wa radi, ambao waganga na wachawi huutumia kuwaadhibu wale wanao wakosea, hasahasa wezi. Pia historia ya kutisha ya Sumbawanga, ndiyo inaifanya sehemu hii kuogopeka na kutajwa kuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Kigoma, mkoa wa Kigoma unashika nafasi ya pili kwakuwa na uchawi zaidi nchini Tanzania. Hii nikwasababu ya matukio kadha wa kadha ya kishirikina yanayotokea mkoani humo kila kunapokucha. Kibondo ndiyo sehemu ambayo inatakiwa kuwa n...
Comments
Post a Comment