Posts

MAGUFULI ATAMBULISHWA ZANZIBAR, AAHIDI KUFUATA NYAYO ZA KARUME NA NYERERE

Image
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema endapo akifanikiwa kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania, ataongoza nchi kwa kufuata nyayo za waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.   Dk. Magufuli alitoa kauli hiyo mjini Unguja, Zanzibar jana, baada kupokewa na mamia ya wananchi kwenye Uwanja wa Ndege wa Karume, huku akiwa na ulinzi mkali tofauti na siku zote.   Alisema viongozi hao waliweka misingi iliyojali kila mtu jambo ambalo limesaidia kuweka umoja, amani, utulivu na mshikamano.   “Nawahakikishia kuwa nitafuata nyayo za waasisi wetu endapo mtanipa ridhaa ya kuongoza Oktoba, mwaka huu.   “Nina deni kubwa kwenu na kwa nchi yangu, eleweni hamtajutia uamuzi wa kunichagua, nitafanya kazi kwa bidii, utii na maarifa kulijenga Taifa hili bila kumbagua mtu yeyote,” alisema Dk. Magufuli              ...

KINGUNGE AENDELEA KUMLILIA LOWASSA, ASEMA SIO FISADI KAMA ANAVYOSEMWA

Image
Mwanasiasa Mkongwe katika medani za siasa nchini Tanzania Kingunge Ngombale Mwiru ameibuka na kuzungumza na Waandishi wa Habari leo  kuhusiana na  mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM uliopelekea jina la Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kukatwa. Akizungumza katika mkutano huo Kingunge amesema   Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika  kuwajadili wagombea  lakini safari hii Kamati ya Maadili imefanya kazi isiyowahusu kikatiba  ikiwemo  kukata majina ya wagombea. Amesema  Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama kwa kujipa madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38. “Kuna baadhi ya watu waliamua kuitumia Kamati ya Maadili kuandaa watu wao na kuwakata wengine kwa sababu zao.”  Amesema Kingunge. Kingunge  amedai kwamba  CCM ni cham...

EMMANUEL MBASHA AKUTWA NA HATIA YA UBAKAJI

Image
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la ubakaji linalomkabili.   Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.   Mbele ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili.   Mbasha ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.   Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.   Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya 20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, ...

KITUO CHA POLISI STAKISHARI KIMEVAMIWA NA MAJAMBAZI NA KUUA POLISI NAKUPORA BUNDUKI AINA YA SMS USIKU WA KUAMKIA LEO.

Image
                 

KINGUNGE ATABIRI ANGUKO LA CCM

Image
Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye ni kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ametabiri anguko na mpasuko mkubwa ndani   chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, endapo chama hicho  kitaacha kumpitisha mgombea urais anayekubalika kwa wananchi wengi. Kauli hiyo imekuja mara baada ya jina la Edward Lowasa kuenguliwa kutoka majina matano  yaliyopendekezwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC- NEC). Kutajwa kwa majina ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Amina Salum Ali, January Makamba na Dk. Asha-Rose Migiro na Kamati kuu kwamba ndio watajadiliwa na Halmashauri Kuu (NEC), kumemfedhehesha Kingunge hata kusema,  “…hatua ya kwanza itakuwa kumweka mgombea ambaye hakubaliki ndani ya chama na hakubaliki nje ya chama. Itakuwa ni kura ya hasira.” Kingunge ametoa kauli hiyo kwa kusitasita huku akionekana kuwa na huzuni wakati akifanya mahojiano na kituo cha Azam Tv   leo mchana .   Japo Kingunge hakutaja jina la Lowassa la...

KUTOKA DODOMA: POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA WAFUASI WA LOWASSA

Image
Wapambe wa Mbunge  wa Monduli Edward Lowassa  hivisasa wanafanya maandamano makubwa nje ya ofisi za CCM hapa makao makuu ya CCM wakipinga Mbunge huyo kuchujwa katika tano bora. Wapambe hao wanaimba nyimbo mbalimbali za kukiponda chama cha Mapinduzi kwa madai kuwa chama hicho  sio cha kindugu  na  pia  sio cha kifalme. Kwa namna nyingine  hali si shwari hapa mkoani Dodoma ambapo sintofahamu imetawala kuhusiana na Edward Lowassa kukatwa. Bado haijulikana nini hatma ya kikao kinachoendelea hivisasa kwa kuwa wa wajumbe wengi wa napinga Lowassa kuchujwa. Baishara zasimama,makao makuu Dodoma. Baadhi ya wapambe wa Lowassa wakipinga Kamati kuu kumchuja Lowassa. Barabara zafungwa Polisi watanda kila kona kudhibiti usalama dhidi ya waandamanaji. Wapambe wa Loawssa wakipinga kukatwa tano bora.

DODOMA KIMENUKA TAZAMA KIPANDE CHA VIDEO HAPA

Image