Posts

KIJUE KILIMO CHA KISASA BILA KUBAHATISHA PIMA UDONGO WAKO SASA

Image
Woote tunajua kuwa kila zao hustawi katika aina flan ya udongo. Sio kweli kuwa kila udongo unakubali mazao yoote je vipi utajua?  Pima udongo wako kwa bei nafuu kujua udongo wako una uchachu uchachu /tindikali kiasi gani (soil ph). Kisha fanya haya hapa:- 1? zalisha zao lenye ph inayolandana na udongo. Au 2? pandisha ph au shusha ph ili iwe sawa sawa na zao lako.  Utapandisha kwa kuweka dolomite au agricultural liming kiasi maalumu kutokana na ukubwa wa shamba lako. (tutakushauri). Kama ni kushusha utaaply sulfur kias maalumu. Hapa ndipo ambapo kila zao litapata virutubisho vyake kama udongo hauna ph husika utakosa virutubisho hivyo. Mazao yatakuwa chini miaka yote na wanashauri usiweke mbolea kwanza kabla hujajua ph je twafanya hivyo? Angalia list hii *PH ZA MAZAO BAADHI* Tomato 5.5-7.5 Onion 6.0-7.0 Watermelon 5.5-6.5 Cabbage 6.0-7.5 Chinese Cabbage 6.0-7.5 Cucumber 5.5-7.5 Rice 5.0-6.5 Sorghum 5.5-7.5 Soybean 5.5-6.5 Spinach 6.0-7.5 Peanut 5....

MAITI YAZUILIWA MUHIMBILI KWA SABABU YA DENI, NDUGU WAOMBA MSAADA

Image
Hospitali ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi Hilda Lukas miaka 30 aliyefariki dunia June 26 katika hospitali hiyo, akisumbuliwa na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha yote wanayomdai marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumia mgonjwa huyo.    Mama wa marehemu Bi Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao, huku gharama za kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi kuongezeka. Maafisaa wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi ya kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa hao. Uongozi wa mtaa wa Chang’ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za kuchangisha wananchi na wadau mablimbali lakini mpaka sasa bado hawajaweza kukamilisha...

MAITI YAZUILIWA MUHIMBILI KWA SABABU YA DENI, NDUGU WAOMBA MSAADA

Image
Hospitali ya Taifa Muhimbili imegoma kuruhusu mwili wa marehemu Bi Hilda Lukas miaka 30 aliyefariki dunia June 26 katika hospitali hiyo, akisumbuliwa na ugonjwa wa utumbo kutoboka huku ikidai lazima fedha yote wanayomdai marehemu ilipwe ambayo ni sawa na shilingi milioni moja na laki moja na nusu kwa mujibu wa ndugu wa familia kama gharama za kumuhudumia mgonjwa huyo.    Mama wa marehemu Bi Anna Zuaro na Bibi wa marehemu wameiomba serikali na wadau mbalimbali kuona namna wanavyoweza kuwasaidia kwani wao mpaka sasa hawana fedha za kuuondoa mwili wa mpendwa wao, huku gharama za kuuhifadhi mwili huo katika chumba cha kuhifadhi maiti zikizidi kuongezeka. Maafisaa wa Muhimbili wanakiri marehemu Hilda Lukas alikuwa amelazwa katika wodi ya kibasira chumba namba 9 ingawa haikuwa rahisi kuzungumza na maafisa hao. Uongozi wa mtaa wa Chang’ombe umesema umefanya juhudi nyingi tu zikiwemo za kuchangisha wananchi na wadau mablimbali lakini mpaka sasa bado...

JOHN MNYIKA AFUNGUKA BAADA YA KIMYA CHA MUDA,AELEZA MSIMAMO WAKE WA KUTAKA LOWASSA AKAMATWE

Image
                                                       John Mnyika (Mb)   Mtakumbuka ni muda sasa sijaonekana wala kusikika katika harakati za kisiasa. Leo nimependa kuweka bayana ili umma wa watanzania ufahamu kwani kumekuwa na upotoshwaji mkubwa juu ya ukimya wangu. Napenda umma wa watanzania ufahamu yafuatayo:- 1. Msimamo wangu wa kuitaka serikali imkamate Mh Edward Lowassa, imhoji na imchukulie hatua kwa mujibu wa sheria kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND haujabadilika kama ambavyo niliwahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA tar 25 Februari 2008 na kipindi chote nikiwa Mbunge wa Ubungo. Hivyo nategemea kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi Lowassa ndiyo atakuwa wa kwa. Siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipoteze ubunge wangu. 2. Sikukubaliana na utaratibu uliotumika kumpata mgombea urais ndani ya Chama ...

ALEX MSAMA AMWANGUKIA MWAKYEMBE BAADA YA GAZETI LAKE LA DIRA KUCHAPISHA HABARI ZENYE UTATA

Image
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki. Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagw a hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari. Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo. Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe. Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo. “Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachuk...

WAZIRI MWAKYEMBE KULISHTAKI GAZETI LA DIRA LILILOANDIKA AMETAPELI BIL. 2

Image
June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi. "Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu "  Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza "Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji  "Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kivita kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kuliti...

MAHAKAMA YAMGOMEA MBOWE, YATUPILIA MBALI KESI YAO YA KUPINGA ZUIO LA POLISI

Image
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.   Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama. Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliyopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi. Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kand...