Posts

DOWNLOAD BURE WIMBO MPYA WA THE SOW BAND( Soul of worship) KUTOKA TANGA

Image

THE SOW BAND - UNYENYEKEVU

Image
                                                Bwana Yesu asifiwe ndugu zetu Watanzania, sisi ni watoto wenu/wadogo zenu/ kaka zenu kutoka Tanga, tumeokoka tunampenda Yesu, na ndio maana tumeamua kumtumikia yeye katika kumsifu na kumuabudu, Tunaimba muziki wa Bendi, na yetu inafahamika kwa jina la THE SOW BAND ambapo ni kifupi cha  SOUL OF WORSHIP. Hivyo basi, tunapoanza kutoa sigle yetu ya kwanza ambayo ni hii inayokwenda kwa jina la UNYENYEKEVU ambayo ipo katika mtindo wa Bolingo (sebene) tunaomba mtupokee na tunaomba mchango wako kwa kwa kutembelea Youtube na kusikiliza audio yetu, kwako wewe kutembelea youtube ni jambo dogo ila kwetu utakuwa umetufanyia kitu kikubwa sana tafadhali usiache kutembelea youtube tunahitaji sana mchango wako bila hakuna THE SOW BAND. Asante sana na Mungu akubariki.

MKATABA TATA WA LUGUMI WATUA BUNGENI

Image
                       Hatima ya mkataba tata wa kampuni ya Lugumi Enterprises ipo mikononi mwa Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya jana, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwasilisha muhtasari wa ilichokibaini baada ya kupitia maelezo ya utekelezaji wake. Moja kati ya mambo yaliyomo katika muhtasari huo ni kulitaka Bunge kutoa ruhusa kwa kamati ndogo iliyoundwa na PAC juzi kuchunguza kwa kina mkataba huo wa kufunga mtambo wa utambuzi wa vidole (AFIS), ikiwa ni pamoja na kutembelea vituo vinavyodaiwa kufungwa mashine hizo. Kamati ya PAC ilinusa ufisadi kwenye mkataba huo wa AFIS ulioitaka Lugumi kufunga mitambo kwenye vituo vya polisi 108 kwa gharama ya Sh37 bilioni lakini ilibainika kwamba kampuni hiyo ililipwa kiasi cha Sh34 bilioni zaidi ya asilimia 90 ya fedha zote ilhali imefunga mashine 14 tu mkoani Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa PAC, Aeshi Hilaly alisema jana muda mfupi baada ya kukutana na ...

HATARI SANA :MCHEZA FILAMU ZA NGONO ALIYEFARIKI AITWA SHUJAA

Image
Aliyekuwa mchezaji mieleka na nyota wa filamu za ngono Chyna amefariki akiwa na umri wa miaka 45. Meneja wake amethibitisha habari hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter. ''Ni masikitiko makubwa kutangaza kwamba tumempoteza shujaa'',ulisema ujumbe huo,akiongezea kuwa:Ataishi kukumbukwa na mashabiki wake wengi na sisi sote tuliompenda. Chyna alipatikana amefariki nyumbani kwake katika ufukwe wa bahari wa Redondo,mjini California,baada ya kurudi nyumbani kutoka Japan. Chyna alipochumbiwa na mchezaji mwenza wa miereka  Mapema wiki hii alichapisha kanda ya video yenye urefu wa dakika 13 ambapo anazungumza kuhusu kuanzisha biashara mpya ya chakula. Alionekana akikosea baadhi ya maneno aliyokuwa akiyatamka na anaonekana amechanganyikiwa. Alijitahidi kukabiliana na dawa za kulevya wakati wote wa kazi yake na alionekana katika kituo cha kuwarekebisha tabia watu maarufu mwaka 2008.

MSANII BONGO MOVIES AFARIKI AKIJIFUNGUA

Image
                                      DAR ES SALAAM : Ni simanzi! Nyota ya msanii Leila Gabriel ‘Lissa’ ambayo ndiyo kwanza ilikuwa imeanza kuchomoza kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, ilizimika ghafla mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya msanii huyo kupoteza maisha muda mfupi baada ya kujifungua kwenye Hospitali ya St. Benard, Kariakoo jijini Dar es Salaam. Filamu alizowahi kucheza? Aishiwa nguvu wakati wa kujifungua. Aabainika kutokuwa na damu ya kutosha. Madaktari washindwa kumfanyia upasuaji Bahati nzuri ajifungua salama. Apatwa balaa lingine baada ya kujifungua, afariki dunia. Mama wa Marehemu afunguka mazito kuhusu kifo cha mwanaye. Simulizi ya kifo chake inasikitisha sana! “Inauma sana, mwanangu amefariki kwa maumivu maana shida ilikuwa ni ambulance, kama ingepatikana kwa wakati naamini angepona lakini ndiyo hivyo tena, kazi ya Mungu haina  makosa,” alisema mama h...

NAIBU MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KUPATIKANA LEO

Image
Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita   Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, anatarajiwa kupatikana leo katika kikao cha kwanza cha Baraza la Jiji kitakachofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee. Uchaguzi wa naibu meya unafanyika baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata meya wa jiji hilo uliohitimishwa Machi 22, mwaka huu kufuatia kutawaliwa na ‘figisufigisu’ kati ya CCM na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) zilizosababisha uaharishwe mara tatu. Katika kinya’nga’nyiro hicho, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita aliibuka kidedea kwa kupata kura 84 dhidi ya Diwani wa Kata ya Mburahati (CCM), Yusuph Yenga aliyepata kura 67. Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita jana alisema  kuwa, maandalizi ya kikao hicho kitakachokuwa na ajenda ya uchaguzi wa kumpata naibu meya yamekamilika. Wagombea nafasi hiyo ni Kafana Mussa wa (CUF) na Mariam Lulida wa CCM. Tofauti na uchaguzi wa meya, uchaguzi wa leo hautarajiwi kuwa na mvutano mkubwa b...

BUNGENI: TANI MILIONI MBILI ZA MUHOGO ZAUZWA KWA DOLA NCHINI CHINA

Image
Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani milioni 2 za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani. Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana  na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM).  Masalla alitaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao. Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China. Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) alitaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.