Posts

MCHAKATO WA URAIS: TANO BORA ITATOKA KWENYE KUNDI HILI HAPA

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya RaisKamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo inakutana kuchuja majina ya makada wake 38 waliorejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia chama hicho na majina 33 ni lazima yapigwe panga ili kupeleka majina matano kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kupigiwa kura. Kwa mujibu wa habari kutoka mitandao ya kijamii, kwenye vijiwe na mijadala sehemu mbalimbali, majina hayo matano yanaaminika kwamba yatatoka miongoni mwa watiania 10 ambao wametajwa zaidi katika mijadala hiyo. Sababu kuu mbili ambazo zimekuwa zikitolewa kwenye mijadala hiyo na hata na baadhi ya wachambuzi wa mambo ya siasa Tanzania ni mbili. Mosi, uzoefu wao ndani ya ungozi wa serikali na pili, nafasi yao ndani ya chama, ama kama wajumbe wa NEC au Kamati Kuu. Majina ambayo yanatazamiwa kwamba yanaweza kupenya Kamati Kuu ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal; Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Kilimo, Chaku...

ROSE MUHANDO AFIKIRIA KURUDI KWENYE UISLAMU

Image
Muimbaji maarufu  wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando. NYOTA   wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza. Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka. Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini. “Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu. “Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose. Mwimbaji huyo amek...

BIASHARA YA NGONO YASHAMIRI DODOMA, MAKAHABA WAJAZANA KILA KONA

Image
BIASHARA ya ngono imeshamiri mkoani Dodoma wakati huu ambao vikao vya kumpata mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimekwisha kuanza.   Uchunguzi uliofanywa  katika baadhi ya kumbi kama  Club Maisha, Club Laazizi na Matei Lounge, Chako ni Chako, umebaini kuwapo idadi kubwa ya kina dada wakiwa wamevaa nusu uchi.   Katika maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma zilikuwapo hekaheka za wasichana wanaojiuza ambao walionekana wakitafuta wateja bila ya wasiwasi wowote na wengine walisikika wakisema  wako kibiashara na siyo kuuza sura.   Eneo maarufu la Chako ni Chako kuanzia jioni mpaka usiku kucha  akina dada hao wamekuwa wakijazana hadi kwenye taa za kuongozea magari huku wakitafuta wateja wenye magari.   Baadhi yao ambao hawakutaka kutaja majina yao halisi mmoja wao alisema,  ‘’Kaka sema una shilingi ngapi habari ya majina unataka kutupeleka wapi…?   ‘’……wewe unaona shimo limetema hapa kila nikigeuka mwanaume...

TCRA YAWAPA ADHABU CHANEL TEN, STAR TV NA TBC

Image
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa adhabu ya faini kwa vituo vitatu vya televisheni nchini kwa kuonyesha vipindi vilivyokiuka kanuni za huduma ya  utangazaji (maudhui ) ya mwaka2005.   Uamuzi huo ulitolewa jijini Dar es salaam jana  na kamati ya Maudhui ya TCRA chini ya mwenyekiti wake Mhandisi Margaret Munyagi ambapo alivitaja vituo hivyo kuwa ni Channel Ten, Star TV na TBC1.   Munyagi alisema ushahidi ulionyesha kuwa vituo hivyo kwa nyakati tofauti na katika vipindi tofauti walikiuka kanuni za Huduma ya utangazaji .    Akizungumzia Kituo cha Channel Ten alisema kimepewa onyo kali na kutakiwa kulipa faini ya Sh Milioni 2.5, kwa kukiuka kanuni  kwa makosa mawili Mei 30 mwaka huu kupitia kipindi cha Kanjanja Time kilichorushwa hewani kuanzia 2:45 hadi 3:10 usiku ambapo walionyesha picha ya mgonjwa akiwa katika wodi ya Hospitali ya Serikali mjini Songea huku sehemu ya makalio yake yakiwa wazi na kuonyesha vidonda.   ...

SHIBUDA AIANDIKIA BARUA KAMATI KUU YA CHADEMA KUOMBA KUKOMA UANACHAMA

Image
Mbunge John Shibuda ameiandikia Kamati Kuu CHADEMA kuomba kukoma uanachama  wake ndani Chama hicho baada ya Bunge kuvunjwa wiki hii.  -Kwa muda mrefu Mbunge John Shibuda amekuwa na mgogoro wa kimyakimya na Chama Chake. Kamatikuu ya Chama imeridhia na kumtakia safari njema,na mafanikio mema huko aendako. ( Tunamshukuru kwa kutumia angalau busara, anaelewa nini maana ya siasa )

MCH. MTIKILA ATANGAZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WASAKA URAIS 6 WA CCM

Image
CHAMA cha Democratic Party (DP) kimetangaza kwenda mahakamani kukishtaki Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na makada wake sita kutokana na kukiuka sheria ya nchi, taratibu pamoja na kanuni za uchaguzi. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa chama hicho Mchungaji Christopher Mtikila, wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema makada hao pamoja na chama chao wamekiuka sheria za nchi pamoja na kanuni za uchaguzi. Aliwataja makada ambao atawaburuta mahakamani kuwa ni Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa pamoja na Frederick Sumaye.   Wengine ni January Makamba, William Ngeleja, Stephen Wassira pamoja na Benard Membe. Alidai makada hao walivunja sheria za nchi pamoja na kanuni za uchaguzi kutokana na kuanza kampeni zao mapema. Alisema  watakishtaki Chama Cha Mapinduzi kutokana na kushindwa kuwachukulia hatua na kuendelea kuwaweka katika mchakato wa kutafuta mgombea wa urais wa chama hicho wakati walishavunja sheria pamoja kanuni za uchag...

MSEKWA: ATAKAYEKATWA AKIONA KAONEWA RUKSA KUHAMA CHAMA

Image
Makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa amesema kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow imekijengea chama hicho chuki kwa wananchi na hivyo kinahitaji mgombea anayekubalika ili kishinde kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.    Msekwa, ambaye ni mmoja wa viongozi wa zamani wanaotarajiwa kutoa mapendekezo yatakayokuwa msingi wa kupata mgombea wa urais wa CCM, alisema hayo kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa kila Jumatatu na Kituo cha Televisheni cha ITV.   CCM imeshaanza mchakato wa mwisho wa kumpata mgombea wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 kwa ajili ya kuwania kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano na pia mrithi wa Jakaya Kikwete kwenye nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho.   Mchakato huo utakamilika Jumapili wiki hii wakati Mkutano Mkuu utakapochagua mgombea wa nafasi hiyo ya juu ya kisiasa nchini.   Akizungumza kwenye kipindi hicho, Msekwa alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, ushindi wa mgombea urais wa CCM, Rai...