Posts

MJAMZITO ACHAPWA VIBOKO NA MUUGUZI, ALAZWA ICU, AMTOTO AFIA TUMBONI

Image
Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni. Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya. Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai. Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy.    “Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdh...

MCHUMBA WAKE KUNASWA KWENYE TUKIO LA UJAMBAZI, MKE MTARAJIWA APASUA JIPU

Image
                          Baada ya mitandao mbalimbali kuripoti habari zinazokinzana juu ya tukio la bwana harusi mtarajiwa aliyetajwa kwa jina la Stephano kunaswa kwenye tukio la ujambazi muda mfupi baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Happy Merere, bi. Harusi huyo mtarajiwa ameibuka na kuanika ukweli wa mambo, Risasi Jumamosi lina full stori. Stephano na wenzake watatu walikamatwa Aprili 21, mwaka huu maeneo ya Red Cross jijini Dar akidaiwa kuhusika katika tukio la kumpora fedha Mzungu mmoja raia wa kigeni pale Kinondoni, Dar. Kwenye tukio hilo, watuhumiwa hao, akiwemo Stephano au mume mtarajiwa wa Happy waliwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi. MITANDAO YAANZA Baada ya tukio hilo kuthibitishwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na watuhumiwa Salum Mtamwa, Alex Makunga, Mohammed Ally na Stephano Kikindi kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi, watu walianza kuripoti tofauti katika mitandao ya kijam...

AUWAWA KWA KUCHOMWA KISU BAADA YA KUKUTWA NA MKE WA MTU

Image
Kijana mmoja kwa jina ADAM MANONDO mkazi wa Sakina auwawa kikatili huko Arusha jana jioni baada ya kufumaniwa akimla mke wa mtu kwenye gari. Mama huyo ni mke wa  mmiliki wa baa moja maarufu jijini Arusha (jina kapuni kwa sasa) na gari walilokuwa wakitumia aina ya VOXY ni la mama huyo.

AFARIKI KWA KUNYWA DAWA ZA KUPUNGUZA UNENE ALIZONUNUA MTANDAONI

Image
                                                                          Eloise Ni binti mrembo wa miaka 21 aliyefikia Chuoni kimasomo ambapo alichukua maamuzi ya kununua dawa za kupunguza/kujikinga na unene alizozinunua kwenye mtandao (online). April 12 2015 ndio ilikua siku yake ya mwisho duniani baada ya kulazwa hospitali na chanzo cha kifo chake kikiaminika ni hivyo vidonge ambavyo inasemekana vilikua na sumu. Mama yake mzazi ameongea na kusema Madaktari wasingeweza kuokoa maisha yake, kunywa hizo dawa ni sawa na kujisogeza karibu na kifo, zinasababisha pia mwili upate joto kupitiliza na kusababisha pia ini kushindwa kufanya kazi. Mama mzazi wa  Eloise Eloise alipoanza kuona hali iko tofauti baada ya kunywa dawa alikwenda hospitali mwenyewe lakini ikawa imeshaharibu taya...

NG'OMBE WALA KONDOO KENYA

Image
          Ng'ombe aliyekula kondoo Kenya Mkulima mmoja nchi Kenya anasema kuwa mmoja wa ng'ombe wake amesusia lishe yake ya kawaida na kuanza kuwala kondoo. Charles Mamboleo, ambaye anamiliki shamba kusini magharibi mwa kaunti ya Nakuru aligungua kuwa ng'ombe wake amemla kondo siku moja asubuni. Jitihada zake za kumpa ng'ombe huyo chakula na maji hazikufua dafu, na siku iliyofuata ng'ombe huyo alimla kondoo mwingine. Kulingana na afisa mmoja wa kilimo ni kuwa , huenda tabia ya ng'ombe huyo huenda imetokana na ukosefu wa madini yanayopatikana kwa mimea mbichi. Hali ya kiangazi ambayo ilimalizika hivi majuzi huenda imesababisha mifugo kukosa madini yanayopatikaan kwenye nyasi mbichi. Mwaka 2007 ndama mmoja nchini India alinaswa kwenye mkanda wa video akila kuku. Source BBC

AFANDE SELE: NIKICHAGULIWA KUWA MBUNGE SITAKUBALI POSHO NA MSHAHARA MKUBWA

Image
Mwana hip hop na Bongo Fleva nchini, Afande Sele, ameweka wazi kwamba hata kama atakuwa mwakilishi wa wananchi katika bunge la mwakani, hataweza kuacha kufanya muziki kwa kuwa ndiyo njia ya kumuingizia kipato.   Alisema licha ya kuwa bungeni, atakuwa akitegemea zaidi fedha zinazotokana na muziki wake badala ya kufikiria mishahara minono na posho zinazopatikana bungeni.   “Kazi yangu ya muziki siwezi kuiacha, ndiyo itakayoniongoza katika maisha yangu, kwa kuwa nitakapokuwa bungeni licha ya kuwa na utetezi mwingine kwa wananchi, lakini pia nitapinga na kukataa posho na mishahara minono wanayopata wabunge kiasi kwamba wanasahau walipotokea,’’ alieleza Afande   Afande, ambaye sasa ni mwanachama wa chama Kipya ya ACT, aliongeza kwamba ili wasanii waweze kuwatumikia vema wananchi, baada ya kuwa wabunge lazima wakatae posho na mishahara minono.   “Wasanii wengi waliopo bungeni wanajisahau kwa kuwa wanapopata posho na mishahara minono wanasahau walipot...

MWILI WA MWANAFUNZI ALIYEFARIKI KWA KUCHAPWA VIBOKO NA MWALIMU WAFIKISHWA DODOMA

Image
MWILI wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Wakati mwili huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu. Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto. "Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili. “Tumechukua uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa hawana vifaa vya uchunguzi vya  kichwa. ...