Posts

KWA NINI ZITTO LEO AMEGOMA KWENDA KUSOMA RIPOTI YA PAC BUNGENI? MAJIBU YAPO HAPA

Image
Wakati  wa  Vurugu  za  Asubuhi  leo  Bungeni, Spika  wa  Bunge  alimtaka  Mwenyekiti wa  PAC, Mh Zitto  Kabwe  aende   kusoma  taarifa  ya  kamati yake.... Kilichotokea  ni  kwamba, Zitto  alitia  mgomo, nikiwa  na  maana  kwamba  alipuuza  agizo  hilo  na  hakunyanyuka  kabisa.   Unajua  ni  kwa  nini? Zitto  Kabwe  mwenyewe  amekwisha  lijibu  hilo  swali  kupitia  ukurasa  wake  wa   Facebook. "Kwa  nini  sikwenda  kusoma taarifa  ya  PAC leo  nilipoitwa  na  Spika? Jibu rahisi  kabisa, siwezi  kuona madhila na uvunjifu  mkubwa  wa  HAKI  za  binadamu  nikaendelea  na  mambo  kama  hakuna  kilichotokea.Kitendo  cha  polisi  kutumia...

BUNGE LA AHIRISHWA TENA JIONI HII, VURUGU ZA ASUBUHI PIA ANGALIA VIDEO YAKE HAPA

Image
Spika wa Bunge Anna Makinda   jioni  hii  amelazimika kuahirisha  tena  kikao cha Bunge hadi kesho asubuhi  kwa  madai  kuwa  serikali  bado  inajipanga  kutoa  majibu  sahihi  kutokana  na  tukio  la  kupigwa  mabomu  Mwenyekiti  wa  Chama  cha  CUF, Profesa  Ibrahim  Lipumba. Kuahirishwa  kwa  bunge  kumetokana na vurugu zilizotokea    leo  asubuhi bungeni baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha  NCCR - Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahimu Lipumba jana akiwa kwenye maandamano . Timbwili  zima  la  vurugu  hizo za  Asubuhi  toka  bungeni  liko  hapo  chini  katika  video.

VURUGU BUNGENI ZASABABISHA BUNGE KUAHIRISHWA LEO

Image
Baada ya Mbatia kuleta hoja ya dharura juu nguvu iliyotumiwa na polisi kwenye maandamano ya CUF jana tarehe 27 January ili ijadiliwe na wabunge kama hoja ya dharura, spika Makinda aliamuru serikali ilete majibu kesho ndio ijadiliwe.  Wabunge walisimama kushinikiza hoja ijadiliwe lakini Makinda aliendelea na msimamo wake wa hoja kujadiliwa kesho baada ya Serikali kuleta majibu, hapo ndipo sintofahamu ilipozidi na kuleta kutoelewana kati ya wabunge wa Upinzani na Spika. Ilibidi spika Anna Makinda kuahirisha bunge mpaka kesho lakini baadae akabadili na kusema saa kumi jioni leo hii.

CLUB OLYMPIA YATEKETEA KWA MOTO

Image
Mwonekano wa lango kuu la Club ya Olympia baada ya kuungua. Askari wa zima moto wakiwa kazini. Sehemu ya ndani ya club hiyo ikionesha majivu ya vitu vilivyoungua . Askari wa zima moto wakiwa kwenye gari lao. Mashuhuda wa tukio wakitazama hasara iliyosababishwa na mto. Askari wa zima moto wakinyoosha mipira ya maji. CLUB   Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.  Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel  Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto. Aliongeza kwamba zima moto  hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako  saa 12 asubuhi wakiwa na maji  kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.

MAGAZETI YA LEO TAREHE 28/JAN/2015 KURASA ZA MBELE NA NYUMA

Image
. . . . . . .. . . . . . . . . . . .

PROF. LIPUMBA,VIONGOZI WAANDAMIZI NA WANACHAMA - WAMEACHIWA KWA DHAMANA

Image
Viongozi na wanachama wote waliokuwa wameshikiliwa hapa CENTRAL POLICE wameachiwa kwa dhamana  na kukabidhiwa vifaa vyao walivyosalimisha awali. Kuripoti tena ni leo saa 4.00 asubuhi. Shukrani za dhati ziwaendee mawakili wa CUF akiwemo wakili msomi  Hashim Bakari Mziray  na wakili mzoefu Job Krario. Pia shukrani kubwa ziwaendee mawakili wengine wawili walioletwa na CHADEMA na mmoja wa NCCR. Tukio hil limeonesha kuwa UKAWA inafanya kazi kama siafu. Mawakili wengine watatu walikuwa njiani kuja hapa CENTRAL tumewarudisha, jumla wangekuwa saba. Kwa uwezo wa mungu HAKI itapatikana siku moja Tanzania. Mabadiliko ni mimi, wewe na yule na yanaanza sasa na yanaanzia kwako na kwangu na kwa yule. Mimi na wewe ndiyo tunawakilisha Tanzania tuitakayo, tuanze sasa na tuendelee kuiunga mkono UKAWA na juhudi zake. Kwa dhati pia niwapongeze Katibu Mkuu wa NCCR, Mosena Nyambabe, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF Joram Bashange, Naibu M...

BINTI HUYU ALIA KWA FURAHA BAADA YA KUMKUTA MAMA YAKE AMEMVALISHA SAA MBWA WAKE

Image