WALAJI WA MBOGA ZA MAJANI JIJINI DAR KIFO KINAWANYEMELEA
Mkulima akichuma mchicha katika shamba lake maeneo ya Keko Mwanga jijini Dar es Salaam. -Hulimwa mabonde ya Msimbazi,Ubungo. -Hatarini kuugua,figo saratani ini na ubongo. Wakazi WA jiji la Dar es Salaam wako katika hatari ya kupatwa na magonjwa makubwa kama saratani, utasa, kupoteza uwezo wa kuona, kuharibu ubongo, maini na figo, kutokana na matumizi ya mboga za majani zinazolimwa katika mabonde ya jiji hilo, NIPASHE imebani Matumizi ya mboga hizo ni makubwa jijini humo, yakitokana na umuhimu wake kwa afya za watu na hali duni ya maisha inayozifanya familia nyingi kumudu gharama zake ikilinganishwa na vitoweo vingine. Sehemu kubwa ya mboga hizo inatokana na kilimo kinachofanyika kwenye bonde la Mto Msimbazi na maeneo ya Kigogo-Sambusa, Ubungo--Gereji, Mchicha – Vingunguti na Tandale. Tayari matokeo ya tafiti kadhaa yamedhihirisha maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mboga za majani jijini humo kuwa na kemikali zenye sumu ama taka zinazotoka viwandani na kwenye ma...