Posts
Showing posts from March, 2016
PICHA: RAIS MAGUFULI AKIWAAPISHA WAKUU WA MIKOA WAPYA LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
- Get link
- X
- Other Apps
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi,Zelote Steven Zelote kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu kuwa mkuu wa mkoa wa Kagera,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga kuwa mkuu wa mkoa wa Katavi,Hafla hiyo fupi ya kuwaapisha Wakuu hao wa Mikoa imefanyika leo Ikulu,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga
WASIFU WA KATIBU MKUU WA CHADEMA DR. VICENT B. MASHINJI
- Get link
- X
- Other Apps
Professional experience Clinical Advisor & TB/HIV lead UMSOM-IHV July 2008 - Present ART Program Doctor/IMA team lead IMA Worldhealth August 2006 - June 2008 (1 year 10 months) Medical Officer/Anaesthesiology Regency Medical Centre October 2005 - August 2006 (10 months) Medical Officer Muhimbili National Hospital August 2003 - October 2005 (2 years 2 months) Research Assistant Freelance November 2002 - August 2003 (9 months) Intern Docor Muhimbili National Hospital September 2001 - October 2002 (1 year 1 month) Education history Open University of Tanzania PhD August 2010 - Present AMREF/UCLA Anderson School MDI Certificate April 2010 - April 2010 Blekinge Institute of Technology MBA September 2007 - March 2010 (2 years 6 months) UMSOM-IHV IPEP Certificate May 2008 - May 2008 Evin School of Management Certificate in CSR October 2005 - October 2005 Muhimbili University College of Health Sciences MMed/Anaesthesiology September 2003 - April 2005 (
JOB NDUGAI ATOA KIBALI CHA KUKAMATWA MBUNGE USIKU WA MANANE
- Get link
- X
- Other Apps
VIONGOZI WA CHADEMA WAANZA KUWASILI MWANZA
- Get link
- X
- Other Apps
Viongozi wa ngazi ya juu wa Chadema wameanza kuwasili jijini Mwanza ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika vikao vya juu vya chama hicho. Leo, wajumbe wa Kamati Kuu wakiongozwa na Mwenyekiti, Freeman Mbowe watawasili jijini Mwanza. Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari wa Chadema, Tumaini Makene ilieleza kuwa Kaimu Katibu Mkuu, Salum Mwalim ameshawasili na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika na wakurugenzi wengine walitegemewa kuwasili muda wowote kwa ajili ya kikao cha Sekretarieti inayokutana kabla ya kile cha Kamati Kuu inayoketi kwa siku mbili kuanzia leo. Baada ya kuwasili jijini Mwanza, Mwalimu alikutana na waratibu wa kanda zote za chama hicho ambako alipokea taarifa fupi ya maandalizi ya awali ya vikao vya Sekretarieti, Kamati Kuu na Baraza Kuu ambalo litaketi Machi 12 kisha kufuatiwa na kikao kingine cha Kamati Kuu Machi 13 asubuhi na jioni kutakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Furahisha. Machi 14, sekretarieti itakutana tena kuhitimisha
ATUPWA JELA MIAKA 7 KWA KUMKATA MKEWE SEHEMU ZA SIRI ILI APATE UTAJIRI
- Get link
- X
- Other Apps
Mkazi wa Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za kishirikina ili apate mali. Hakimu Joctan Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka. Hakimu Rushwela alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina. Awali wakili wa Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya Mbugani, Manispaa ya Tabora. Wakati wa tukio hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata Sh5milioni. Alidai baada ya kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze kutimiza ukatili h
MASHABIKI WA REAL MADRID WAMZOMEA CHRISTIANO RONALDO
- Get link
- X
- Other Apps
Licha ya kufunga goli ambalo limesaidia kwenye ushindi wa Real Madrid Vs Roma kwenye UCL, mashabiki wa Real Madrid wamemzomea mchezaji wao muhimu Cristiano Ronaldo.. Baada ya kitendo hicho kutokea Sergio Ramos moja kwa moja alikua upande wa Ronaldo na kusema kwamba, “Ningependa kuwaambia mashabiki kufikiria kidogo,ninawaheshimu sana lakini vitu visipoenda vizuri inabidi muda wote wawe upande wa wachezaji wao. Mafanikio kwa club ndio kitu ambacho wachezaji wote tunataka. Ronaldo ni mchezaji wa ki historia kwenye kikosi cha Real Madrid, anaendelea kuonyesha ubora kila mwaka” Ronaldo anasema kwamba alikua qouted vibaya alivyosema wachezaji wenzake wangekua level kama yake basi wasingepoteza mechi dhidi ya Atletico Madrid. Kauli hiyo ndiyo imesababisha mashabiki kumzoea wakiitafsiri kwamba ni kudharau wenzake lakini yeye anasisitiza kwamba alimaanisha wengi walikua na injury lakini yeye hakuwa nayo.
MWAMUZI ALIYECHEZESHA SIMBA VS YANGA, SASA KUCHEZESHA KOMBE LA DUNIA
- Get link
- X
- Other Apps
Jonesia Rukyaa-Mwamuzi aliyechezesha pambano la VPL Yanga vs Simba February 20, 2016 Mwamuzi wa kike wa Kimataifa wa Tanzania mwenye beji ya FIFA, Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuungana na waamuzi kutoka nchini Kenya kuchezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (WWC-Q 17) mwishoni mwa mwezi huu. Jonesia Rukyaa atakua mwamuzi wa akiba katika mchezo huo kati ya Misri dhidi ya Cameroon utakaochezwa jijini Cairo wikiendi ya tarehe 25,26,27 Machi, 2016. Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakua ni Carolyne Wanjala (Kenya), akisaidiwa na Carolyne Kiles (Kenya), Mary Njoroge (Kenya), huku kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Leah Annette Dabanga kutoka nchi ya Afrika ya Kati. Imetolewa na shirikisho la soka Tanzania (TFF)
MKUTANO MKUU TFF KUFANYIKA JIJINI TANGA
- Get link
- X
- Other Apps
Mkutano Mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike mwezi Disemba mwaka jana sasa utafanyika wikiendi hii Jumamosi na Jumapili tar 12-13 March 2016 jijini Tanga. Ajenda za mkutano huu ni kwa mujibu wa katiba ya TFF. Mkutano mkuu utahitimishwa kwa uwekaji wa jiwe la msingi la kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji vya uchezaji mpira, kituo kitakachojengwa jijini Tanga. Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Regal Naivera. Imetolewa na shirikisho la soka Tanzania (TFF)
BOBAN NJE MBEYA CITY
- Get link
- X
- Other Apps
Kiungo Haruma Moshi Boban atalazimika kusubiri mpaka March 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City kufuatia kusumbuliwa na maralia jambo linalomfanya kuukosa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Stand United ya Shainyanga uliopangwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa. Muda mfupi uliopita mkuu wa kitengo cha utabibu kwenye kikosi cha City, Dr Joshua Kaseko ameifahamisha mbeyacityfc.com kuwa mara baada ya kikosi kizima kurejea Mbeya kutoka jijini Dar kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba, alipata taaraifa ya kutokuwa katika hali nzuri kwa kiungo huyo na baada ya kumfanyia vipimo aligundua kuwa Boban ana Maralia. “Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo kesho,ana Maralia tumeshamtaarifu mwalimu juu ya hili na tayari ameanza kufanya mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans Sports jijini Tanga alisema. Katika hatua nyingine Dr Kaseko alid
PICHA ZA AZAM FC WAKIWA WANAELEKEA SOUTH AFRICA KUCHEZA NA BIDVEST WITS
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS TUONG WA VIETNAM LEO
- Get link
- X
- Other Apps
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, kwa ajili ya mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Rais huyo yupo katika ziara ya kikazi nchini. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji na Waziri Mahiga. Rais Truong wa Vietnam akimsifia jambo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati akimuaga baada ya mazungumzo yake na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kulia) Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa katika mazungumzo ya pamoja na viongozi wengine na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang na ujumbe wak