Posts

Showing posts from May, 2015

UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID ULIVYONOGA KUSUBIRI LOWASA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

Image
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha jijini katika maandalizi ya Mkutano wa Edward Lowassa.    Muonekano wa uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.    Wamasai wakitoa burudani katika maadalizi ya mkutano wa Edward Lowassa.   Akina mama wa Kimasai katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.    Baadhi ya wananchi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha   Leo Mbunge wa Monduli Edward Lowassa atatangaza nia ya kugombea Urais katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  jijini Arusha.Maandalizi mbalimbali yanaendelea huku ilinzi ukiimarishwa kila kona.   Mamia ya wananchi wanaendelea kuingia katika uwanja huu kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo Dares salaam,Arusha,Dodoma,Kagera,Mwanza na Mbeya   Kila mtu katika uwanja pamoja na Watanzania wana shauku ya kutaka kufahamu Edward Lowassa atasema nini kuelekea katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika wiki ya mwisho ya mwezi oktoba mwaka huu 2015.  

TAHADHARI PICHA ZA KUTISHA; MADHARA YA NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA

Image
Ni hivi karibuni Serikali kupitia mamlaka zake zinazohusika na Maswala haya ya nguo za mitumba ilipiga marufuku huuzwaji wa Brazia,Nguo za Ndani za mitumba kuuzwa kwa wananchi kwa sababu zinaelezwa si salama kwa asilimia mia moja,na misako mbalimbali ilifanyika kwenye maeneo maarufu kwa kuuza aina hiyo ya Nguo lakini baadhi ya wananchi ama kwa kudharau matamko yanayotolewa na Serikali pamoja na wahuzaji waliendelea kufanya biashara hiyo kwa hiyo ni wito wetu kwenu mwambia Dada,Mpenzi wako,Shangazi,Rafiki yako na mtu yeyote yule kuwa Nguo hizi za Mtumba Brazia,Nguo za ndani hazifahi na haya ndio madhara yake ukipenda  . PIGA VITA UTUMIAJI HUU WA BRAZIA,NGUO ZA NDANI ZA MITUMBA SIO NZURI!

AAMBUKIZA UKIMWI WANAFUNZI 712 WA VYUO VIKUU.!

Image
 Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Rogers (pichani) raia wa Uganda amekiri kufanya ngono na wanafunzi 712 wa vyuo vikuu mbalimbali nchini Tanzania na Uganda na kuwaambukiza virusi vya UKIMWI kwa kipindi cha miaka mitatu. Rogers amesema alipogundua ana maambukizi ya HIV mwaka 2012 aliamua kulipiza kisasi kwa kuambukiza wasichana wengi kadri iwezekanavyo. Hadi kufikia mwaka huu alikwisha ambukiza wasichana 712 wote wakiwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Tanzania na Uganda. Vyuo vya Tanzania ambavyo Rogers anadai kutembea na wanafunzi wake ni CBE(7) Dar, IFM(10), USTAWI(10), UDSM(35)na TIA(4) Pia amedai kuwa kati ya wasichana wote 712 aliotembea nao hakuna yeyote aliyemrudia mara mbili wala kutumia condom. "Sikuhitaji kumrudia mtu mara mbili maana ni kupoteza muda. Nilijitahidi kadri niwezavyo kuwapata wengi ili kutimiza azma yangu ya kuambukiza mamia ya wanafunzi." alisema Rogers. Mmoja kati ya wasichana ambao Rogers ametembea nao na kumuambukiza virus

REST IN PIECE MY LOVELY UNCLE/DAD ROY DAVID SEBARUA

Image

WADADA/WAMAMA MNAJUA MAWIGI NA "MAWIVINGI" YALE ORIGINAL YANAVOPATIKANA? INGIA HAPA.

Image
There is nothing wrong with moderately wearing hair extensions although some may argue that our doing so means we do not appreciate what God has already done and we are trying to perfect on His work. But many Christians today are putting themselves in bondage by wearing the so called human hair “Remi” extensions and wigs in place of their own hair.  It may look all beautiful outwardly but basically you can decorate your glory by wearing a bunch of snakes on your hair. The kingdom of darkness has invented yet another way of putting many people in bondage and many Christians are blind to this. Tonsuring or “Sacrificing Beauty” Tonsuring also known as “sacrificing beauty” has lead a multi-million dollar industry for those seeking for results. Sacrificing beauty is shaving ones hair and sacrificing it to hindu gods in hopes that the problem for which they are sacrificing their hair will be solved. Thus after the hair is shaved off, it is sacrificed to the hindu

KAMATI NIDHAMU YA TFF YAMPIGA FAINI YA MILION 5, AFISA HABARI WA KLABU YA YANGA JERRY MURO

Image
                   Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF. Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa.. Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo. Source Global publishers

LULU AKANA KUWA NA JINI MAUTI

Image
MSANII nyota wa filamu, Elizabeth Michael `Lulu’ amekanusha uvumi kuwa matatizo yanayowatokea wanaume aliowahi kuwa nao yanatokana na yeye kuwa na Jini Mauti anayesababisha hali hiyo kutokea, Amani linakujuza. Akizungumza na Gpl juu ya madai ya wadau mbalimbali kuhusiana na matukio mengi yanayomtokea, muigizaji huyo wa filamu ya Foolish Age, alisema maisha yake ya siku hizi ni ya kusali sana, hivyo anaamini kutokana na maombi yake, hali yake iko vizuri kutokana na Mungu kumpa anachokihitaji.   “Ninasali sana kwa sasa aisee, mara nyingi nafanya hivyo mara tatu kwa siku, ninao uwezo wa kukemea mapepo na yakaondoka, hayawezi kukaa mwilini mwangu,”  alisema muigizaji huyo ambaye miaka michache iliyopita, aliondokewa na mpenzi wake, Steven Kanumba aliyeanguka na kufariki mbele yake.   Mtabiri mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, Maalim Hassan Yahya Hussein, alisema tatizo kubwa linalomsumbua binti huyo ni jini mauti ambalo baada ya kumpenda, halitaki kuridhia uhusiano wake w

MREMA AVULIWA UANACHAMA TLP

Image
KAMATI ya Ukweli na Maridhiano ya Chama cha Tanzania Labour (TLP), imetangaza kumvua uanachama Mwenyekiti wa chama hicho, Agustino Mrema.   Akizungumza jana, jijini Dar es Salaam na vyombo vya habari, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joram Kinanda alisema kuwa kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia kwa kina malalamiko yaliyokuwa yakimuhusu Mrema, ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo.   Mwenyekiti huyo alisema kuwa mbali na Mrema wengine waliovuliwa uanachama ni Hamisi Mkadamu, Antoni Mapunda, Nancy Mrikaria, Dominata Rwechungura, Maxmilian Lymo, Richad Lyimo, Hamisi Mkumba na Stanley Temba.   Kinanda alisema kuwa wanachama hao wamevuliwa uanachama kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, toleo la 2005 Ibara ya 9.9 (c) na 2009 ibara 9.5(c).   Kinanda alisema kuwa maazimio hayo yamepelekwa katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kwa taratibu za kisheria pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).   Kwa upande wake Msajili Msaidizi wa Vyama Vya Siasa nchini, Sisty Nyah

INTERVIEW YA GAZUKO NA KIANGO RADIO

Image
                  Gazuko ni miongoni mwa wanagospel hip hop ambaye ni Group A kwa Tanzania kwa maana hauwezi kuzungumzia Gospel hip hop bila kumzungumzia Gazuko hivyo tumia dakika chache kufuatilia mahojiano yake aliyofanya na Kiango Radio.

MTOTO ATOA USHUHUDA UNYAMA ALIYOFANYIWA BABA YAKE NA POLISI BAADA YA KUMGONGA

Image
Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support ya jijini Dar, Octavian Nandi Mpendakazi. Askari wa Kampuni ya Ulinzi ya Knight Support ya jijini Dar, Octavian Nandi Mpendakazi (60), hali yake ni mbaya kwa kile kinachodaiwa aligongwa na gari la polisi na kuvunjika mbavu, mguu wa kushoto mara mbili pia kakatika utumbo siku ya Sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Mtoto wa majeruhi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rose Nandi, akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, alidai kwamba baba yake aligongwa na gari la polisi wakati akivuka barabara Aprili 26, mwaka huu eneo la Tazara, Dar. “Nilipoenda eneo la tukio niliambiwa na walioshuhudia kwamba baba aligongwa na ‘defender’ la polisi,” alisema mtoto huyo.Aliendelea kusema kwamba, baba yake aligongwa saa kumi na mbili na nusu asubuhi na gari hilo lililokuwa likitokea Gongo la Mboto kwenda Uwanja wa Taifa kwenye sherehe za Muungano. “Siamini kama baba atapona na hata kama atapona lakini tayari wameshamtia ulem

YALIYOJIRI KWENYE MAGAZETI YA LEO TAREHE 06/05/2015

Image

YESU OKOA MITAA NA USIKU WA VIPAJI

Image
   KWA MARA NYINGINENI IJUMAA HII #YESUOKOAMITAA  WANAKULETEA USIKU WA VIPAJI,USIKU ULIOJAA KILA AINA ZA VIPAJI AMBAO UTAFANYIKA IJUMAA HII YA TAREHE 8-5-2015 KATIKA KANISA LA TAG SEGERA CHAMA KWA MCHUNGAJI BONVENTURE KATEMBO KUANZIA SAA TATU USIKU HADI ASUBUHI...WATU WOTE MNAKARIBISHWA BUREEEE HAKUNA KIINGILIO . USIKU HUO UTASINDIKIZWA NA TIMU NZIMA YA YOM NA KWAYA MBALIMBALI USIPANGE KUKOSA MAANA  NI USIKU WA KIHISTORIA....PIA MCHUNGAJI KATEMBO ATAKUFUNDISHA KIPAJI CHAKO KILIVYO MTAJI WENYE NGUVU KWENYE MAISHA YAKO....JINSI YAKUFIKA PANDA MAGARI YA TABATA SEGEREA WAAMBIE WAKUSHUSHE SEGEREA CHAMA HAPO HAPO LIPO KANISA .TUPIGIE KUPITIA NAMBA #0712 348032 KUPATA MAELEZO ZAIDI ...CHAI KAHAWA BITES VYOTE VITAKUWEPO...YESU OKOA MITAA KILA KONA YA MTAA...YOM-DAIMA  

SHUKA YAMUUA MUENDESHA BODA BODA

Image
MKAZI wa Kijiji cha Ndeleta kilichopo wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, Saria Kidali (47), amefariki dunia baada ya kunyongwa na shuka alilokuwa amejifunika wakati akiendesha pikipiki. Tukio hilo la aina yake lilitokea jana asubuhi wakati Kidali alipokuwa akitoka shambani kwake Nadosoiti.   Kabla ya kifo hicho, shuka ya mwendesha pikipiki huyo ilinasa kwenye tairi ya nyuma na shuka hiyo kumbana shingo Kidali hadi alipopoteza maisha baada ya kudondoka chini. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuitaja pikipiki iliyomuua Kidali kuwa ni aina ya Toyo yenye namba za usajili T613 BEB. “Pikipiki hiyo inasemekana ni mali ya marehemu na taarifa za awali zinaonyesha chanzo cha kifo hicho ni shuka alilokuwa amevaa kwani lilijizungusha kwenye tairi na kumnyonga shingo,”  alisema Kamanda Fuime. Pamoja na hayo, alitoa wito kwa waendesha pikipiki kuchukua tahadhari wakati wote ili kuepukana na ajali zinazoweza kuepuki

UPELELEZI KESI YA GWAJIMA MBIONI KUKAMILIKA

Image
UPELELEZI wa kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Mchungaji  Josephat Gwajima na wenzake watatu unadaiwa uko mbioni kukamilika.   Taarifa hiyo iliwasilishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro mbele ya Hakimu Mkazi Frank Moshi wakati kesi hiyo ilipotajwa.   Wakili huyo alidai kesi hizo zililetwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake upo mbioni kukamilika hivyo anaomba ziahirishwe waweze kukamilisha.   Hakimu alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hizo hadi Juni 4 mwaka huu.   Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Msaidizi wa askofu huyo,  Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mzava (43) na Mkazi wa Kimara Baruti Geofrey Milulu (31).   Katika kesi ya kwanza namba 85,Gwajima anadaiwa kwamba kati ya Machi 16 na 25 mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika Pekas alitoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu wa Kanisa Katoliki Muwadhama Policapy Kardinaly Pengo.  

SOFIA SIMBA: RAIS KIKWETE HAJASAINI MSWADA WA SHERIA YA MTANDAO, LAKINA SIO MREFUI ATAUSAINI MUD

Image
Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi Taasisi ya maendeleo ya jamii ya Sitti Tanzania Foundation iliyofanyika Dar es Salaam juzi (kushoto) ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Sitti Mtemvu. Na Mwandishi Wetu, Mpekuzi-Dar es Salaam WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, amesema kuwa kutokana na hali ya nchi kwa sasa Rais Jakaya Kikwete, atasaini sheria ya mtandao.   Kauli hiyo aliitoa jana  baada ya kuripotiwa na gazeti moja la kila siku mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Kitabu cha Chozi la Sitti, ambapo alinukuliwa akisema kuwa Rais Kikwete ameshasaini sheria hiyo.   Akikanusha taarifa hiyo alisema kuna uwezekano amenukuliwa vibaya ila usahihi wa kile alichosema ni kwamba Rais ataisaini sheria hiyo kutokana na hali ya usalama wa nchi kwa sasa.   “ Nilishosema si kwamba sheria imesainiwa,  maana kwa mujibu wa utaratibu wa sheria ni kwamba sheria yoyote rais akishaisaini inapelekwa taari