Posts

Showing posts from October, 2016

(VIDEO) BADDIE WINKLE BIBI WA MIAKA TISINI ALIYEKATAA KUZEEKA

Image
Helen Ruth Elam Van Winkle  a.k.a  Baddie winkle  (alizaliwa July 18, 1928 katika mji wa   Hazard ,  Kentucky ), ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii mwenye follwers wengi kwenye instagram facebook na twitter Baddie winkle aliyendika kwenye Bio yake kwenye mitandao ya kijamii inayosema '' Stealing Your Man Since  1928'' ndio mwana mama mzee zaidi Duniani aliyekataa kuzeeka na kuendelea kula bata huku akiwa na nguvu  ANGALIA HAPA VIDEO YA  BADDIE

(VIDEO) MTU MREFU KULOKO WOTE DUNIANI ALIPOKUTANA NA MTU MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI

Image
Sulatan Kosen mtu mrefu kuliko wote Duniani He Pingping akipozi na kiatu cha mtu mrefu kuliko wote duniani

LIPUMBA AFUNGUA AKAUNTI MPYA YA RUZUKU CUF, NMB WALAUMIWA KUVUJISHA SIRI

Image
Siri kwamba Profesa Ibrahim Lipumba amefungua akaunti mpya yenye jina la chama cha Wananchi CUF imefichuka. Wanaolaumiwa kutokana na kufichuka kwa siri hiyo ni watumishi wa benki ya NMB tawi la Ilala. Prof. Lipumba ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa huku chama chake kikiwa tayari kimemfukuza uanachama. Abdul Kambaya, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma anayetambulika na Msajili wa Vyama Vya Siasa pia huku Baraza Kuu la Uongozi la CUF likiwa limemsimamisha uanachama, amenukuliwa na gazeti la Tanzania Daima, akilaani kitendo cha benki ya NMB kuvujisha taarifa za akaunti mpya ya Prof. Lipumba. “Aulizwe Meneja wa NMB Ilala, kutoa siri za wateja, hayo ndiyo maadili ya kazi yake? Uko wapi usiri kati ya mteja na benki?”  alihoji Kambaya. Hata hivyo, alipotafutwa Kambaya  ili kufafanua uanzishwaji wa akaunti hiyo, matumizi yake na kama yamezingatia matakwa ya Katiba ya CUF na Sheria ya Vyama Vya Siasa, hakuwa tayari kufafanua

HOTUBA YA MH. ZITTO KATIKA MKUTANO MKUU WA KIDEMOKRASIA

Image
Ndugu Mama Anna Elisha Mghwira, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wazalendo, Ndugu Viongozi wote wa chama katika ngazi mbalimbali Ndugu Wanachama Ndugu wageni waalikwa Ndugu wananchi Mabibi na Mabwana Karibuni Sana! Ninayo furaha na heshima kubwa kusimama mbele yenu na kuhutubia kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Kwanza wa Kidemokrasia wa Chama chetu. Mkutano wa kidemokrasia ni kikao pekee rasmi cha kikatiba katika chama chetu ambapo viongozi na wanachama wanakutana ana kwa ana na kubadilisha mawazo kuhusu chama na maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla. Aidha, katika mkutano huu tunawaalika wageni mbalimbali kutoka nchi na vyama marafiki kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika nyanja mbalimbali. Mkutano wa Kidemokrasia ni kikao cha aina yake kwa kuwa wanachama na waalikwa wengine wanahudhuria kwa hiari yao na kwa gharama zao. Muhimu zaidi ni kwamba katika kikao hiki hata wananchi wasio wanachama wanakaribishwa kuhudhuria ili wasikilize na kushiriki kutoa maoni ku