Posts

Showing posts from June, 2016

ALEX MSAMA AMWANGUKIA MWAKYEMBE BAADA YA GAZETI LAKE LA DIRA KUCHAPISHA HABARI ZENYE UTATA

Image
MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba,  Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki. Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagw a hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari. Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo. Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe. Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo. “Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari,  ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi

WAZIRI MWAKYEMBE KULISHTAKI GAZETI LA DIRA LILILOANDIKA AMETAPELI BIL. 2

Image
June 21 2016 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na utapeli. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi. "Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu "  Amesem a waziri Mwakyembe na kuongeza "Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji  "Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kivita kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kuliti

MAHAKAMA YAMGOMEA MBOWE, YATUPILIA MBALI KESI YAO YA KUPINGA ZUIO LA POLISI

Image
KESI ya madai iliofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ya kuiomba mahakama kupiga marufuku zuio la Polisi, leo limetupiliwa mbali.   Mbowe alifungua kesi hiyo namba 79 ya mwaka 2016, baada ya hivi karibuni Jeshi la Polisi  kupiga marufuku mikutano ya hadhara kwa madai kwamba, hali ya usalama nchini si salama. Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, Kilimanjaro katika shauri hilo, aliwashtaki Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kwa madai wanahusika kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, walitangaza kufanya oparesheni iliyopewa jina ‘Okoa Demokrasia nchini’ iliyokuwa na lengo la kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kile alichodai, kuendesha nchi bila kufuata katiba ya nchi. Hata hivyo, baada ya kupigwa marufuku kwa maandamano, Mbowe alifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwan

TCRA WAMEFANIKIWA KUZIMA SIMU LAKI SITA (600,000) ZOEZI LINAENDELEA

Image
Uzimaji wa Imei bandia ulifanyika usiku wa kuamkia jana kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) katika simu zaidi ya 600,000 zenye Imei batili.  Kwa mujibu wa TCRA, Imei ni namba ya kimataifa ya utambuzi wa vifaa vya kielektroniki, ikiwamo simu. Ina tarakimu 15 ambazo ni za kipekee kwa kifaa husika na zinatambulika kimataifa. Namba hizo hutumika kudhibiti bidhaa bandia au simu kutumiwa na mtu mwingine.  Jana, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema takwimu hizo ni zile ambazo zimetokana na kazi ya kukata mawasiliano katika simu bandia iliyofanyika kuanzia saa sita usiku mpaka saa kumi alfajiri ya jana.  Alisisitiza kuwa mtambo huo unaendelea na kazi kuhakikisha kuwa hata simu ambazo hazipo au hazikuwa hewani zitakapowashwa hazitafanya kazi. 

ALIYEMTUKANA RAISI MAGUFULI AKABIDHIWA MIL 4.5

Image
Wanaharakati na wadau wa mitandao ya kijamii nchini wamemkabidhi Sh4.5 milioni aliyekutwa na hatia ya kumtukana Rais John Magufuli ili akalipe faini aliyotakiwa atoe na mahakamani kuepuka kifungo cha miaka mitatu. Mshtakiwa huyo, Isaack Habakuki alikutwa na hatia baada ya kukiri kosa la kumtukana Rais kupitia ukurasa wake wa facebook. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imemtaka kutoa Sh 7 milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.   Mratibu aliyekuwa anakusanya michango hiyo kwa Kanda ya Kaskazini,  Diwani wa Levolosi,  Ephata Nanyaro amesema jana kuwa  wamefanikiwa kupata michango hiyo kupitia makundi ya mitandao ya kijamii waliyoyaanzisha. "Lengo ni kumsaidia mwenzetu kwa kuwa kupitia sheria hii ya mitandao tunaamini hakuna aliyesalama na sheria hii itawagusa wote, "  amesema Nanyaro. Naye,  Habakuki amewashukuru Watanzania waliojitolea kumchangia akisema kupitia adhabu hiyo atakuwa wa kwanza kufundisha jamii kuhusu sheria za mitandaoni

TAARIFA YA ACT- WAZALENDO KUHUSU KUPOTEA KWA NDUGU ZITTO Z KABWE

Image
TAARIFA KWA UMMA Tunaujulisha UMMA kwamba Kiongozi wa Chama chetu cha ACT Wazalendo ndg. Zitto Kabwe amekuwa anatafutwa na Polisi tangu jana usiku. Mpaka sasa hatujui Kiongozi wetu yupo wapi na yupo kwenye Hali gani. Askari kanzu wanalinda nyumbani kwake na kwa watu wake wa karibu.  Sisi kama chama tunaliambia jeshi la Polisi kuwa lolote litakalotokea kwa Kiongozi wetu wao watajibu kwa umma.   Msafiri Mtemelwa,  Kaimu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo

KILIMO BORA CHA MATANGO

Image
Utangulizi Matango ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na hustawi vyema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo   Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji Maandalizi ya shamba  Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi 1.5 kutoka kati ya tuta na tuta Upandaji  Zipo aina mbili za upandaji,  kupanda mbegu moja kwa moja na kupanda mbegu katika trei na kuhamisha baada ya siku 8 hadi 10. Njia ya kupanda mbegu moja kwa moja ni rahisi lakini ile ya kupanda katika trei ni bora zaidi kwani shamba hujaa vizuri katika nafasi na hukua haraka na kuzaa mavuno mengi. Pima mashimo ya kupandia katika umbali wa sentimita 20 hadi 25 kutoka shina hadi shina mstari mmoja kwa tuta na sentimita 40 katika mfumo wa zig-zag pande zote mbili za tuta na kupanda. Mbolea kianzio iwekwe katika kila shimo na kupanda endapo miche kutoka katika trei